TANZIA Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Bugozi Musuguri afariki dunia

Asante sana Chief Manyerere kwa taarifa hii na andiko hili。
P
 
Dah hv vibint sasa
Huwezi amini nikiwahi kukutana na huyu CDF pale Seronera Serengeti akiwa na hao mabinti. Nilimwamkia Jambo Afande CDF Mstaafu. Kisha nikawageukia wale niliodhami ni mabinti, nikawaambia " Mabinti hamjambo" Afande CDF Musuguri akasema hawa siyo mabinti ni MAMA ZAKO WAAMKIE. Kwa shingo upande nikawaamkia SHIKAMOONI Mama zangu. Walibaki kucheka tu.
 
Ukatii agizo.Safi kabisa.
 
Kumbe hata Nyerere alikuwa mkabila?
 
Acha uongo umasikini wa Tanzania ni tatizo linalotokana na mabadiliko ya mfumo kutoka Ujamaa kwenda ubepari,na ulifanyika makusudi na USA ili kuzididimiza nchi zilizokuwa zinafuta Sera za ujamaa.
 
Kumbe hata Nyerere alikuwa mkabila?
Sio ukabila Mkuu wa majeshi ndii kila.kitu ukimuweka mtu ambaye humwamini na kumfahamu vizuri,utapinduliwa kesho tu.
Wewe unadhani Marais wanpo safari kwenda Nje,nchi huwa anaachiwa nani?????
Kiutendaji ataachiwa Makamu au Waziri Mkuu,but kiuhalisia huwa aanachiwa Mkuu wa majeshi.
 
Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali David Musuguri amefariki dunia leo Oktoba 29, 2024 akiwa na umri wa miaka 104 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu, familia imethibitisha.

Jenerali Musuguri atakumbukwa kwa jinsi alivyoongoza vikosi vya Tanzania kwenye vita ya Kagera dhidi ya Idd Amin Dada mwaka 1979.

Vita hiyo ilitokana na uvamizi aliofanya Idd Amin katika Mkoa wa Kagera, jambo ambalo Rais wa Tanzania wa kipindi hicho, Mwalimu Julius Nyerere hakukubaliana nao, hivyo akaamuru vikosi vya Tanzania kwenda kumpiga na kumwondoa.

Chanzo: azamtvtz

Ulinipenda sana Mjukuu wako na Marehemu Dada yangu na kila mara ulikuwa hauchoki Kutuulizia kwa Wazazi wetu.
 

Asante kwa kutukumbusha
 
RIP General Musuguri,umekuwa na Utendaji uliotukuka na Ulishiriki Vita kwa Vitendo na sio Elimu,Hakika we ni ICON ya Jeshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…