Mkuu wa Majeshi na Gavana wa Benki Kuu nani ana mkwanja analindwa na Ni nyeti kuliko mwingine

Sijajua nini maana ya kuwa na mkwanja lakini kisheria msahahara na marupurupu ya Gavana yanapangwa na Rais. Hii naona haijatajwa na Sheria kwa CDF ikimaanisha Utumishi ndio hupanga mshahara wake.
Kuhusu kulindwa zaidi sijajua unamaanisha nini maana hata kama unawaongoza mgambo hakuna mtu atakuuliza ukiwafanya wote wawe walinzi wako.. maana yake CDF atatumia wapiganaji haohao kuwa walinzi wake.
Gavana kulindwa itategemea utashi wake tu lakini atalindwa kama maafisa wengine Waandamizi wa Serikali km. kuwa na mlinzi, dereva ambaye anaweza kuwa mlinzi pia.n.k.
Kuhusu unyeti kufuatana na sheria zenyewe Rais lazima ateuwe Gavana wa Benki Kuu lakini siyo lazima ateuwe Mkuu wa Majeshi.. anaweza kuongoza Majeshi yeye kama Amiri Jeshi Mkuu (C-In-C) au akakasimu kwa Kamati ya Jeshi la Ulinzi ( DFC).. Niko tayari kwa ukosoaji wa kujenga..🙂
 
Mkuu wa Majeshi ni mtu muhimu zaidi na analindwa kuliko Gavana. CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, yani majeshi yote hadi usalama wa taifa yapo chini yake. Gavana hamzidi chochote CDF

Sent from my iPhone using JamiiForums
Hakuna jeshi linaloitwa usalama wa taifa,Wala hakuna cheo kinachoitwa mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama .Bali Kuna mkuu wa majeshi ambaye ni kiongozi wa majeshi ya ulinzi ,Wala hausiki na askari polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Majeshi ni mtu muhimu zaidi na analindwa kuliko Gavana. CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, yani majeshi yote hadi usalama wa taifa yapo chini yake. Gavana hamzidi chochote CDF

Sent from my iPhone using JamiiForums

Gavana ni kama manager tu wa bank japo naye lazima analimdwa lakini ulinzi hauwezi kuwa wa kumlinganisha na CDF
sina uhakika sana lakini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijajua nini maana ya kuwa na mkwanja lakini kisheria msahahara na marupurupu ya Gavana yanapangwa na Rais. Hii naona haijatajwa na Sheria kwa CDF ikimaanisha Utumishi ndio hupanga mshahara wake.
Kuhusu kulindwa zaidi sijajua unamaanisha nini maana hata kama unawaongoza mgambo hakuna mtu atakuuliza ukiwafanya wote wawe walinzi wako.. maana yake CDF atatumia wapiganaji haohao kuwa walinzi wake.
Gavana kulindwa itategemea utashi wake tu lakini atalindwa kama maafisa wengine Waandamizi wa Serikali km. kuwa na mlinzi, dereva ambaye anaweza kuwa mlinzi pia.n.k.
Kuhusu unyeti kufuatana na sheria zenyewe Rais lazima ateuwe Gavana wa Benki Kuu lakini siyo lazima ateuwe Mkuu wa Majeshi.. anaweza kuongoza Majeshi yeye kama Amiri Jeshi Mkuu (C-In-C) au akakasimu kwa Kamati ya Jeshi la Ulinzi ( DFC).. Niko tayari kwa ukosoaji wa kujenga..🙂

unaweza kuwa sahihi mkuu maana kuna nchi hazina mkuu wa majeshi, rais anakua ndiye CDF,RAIS,AMIRI JESHI nk ila GAVANA lazima awepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia majibu ya baadhi ya watu wa humu kwenye hii thread unapata picha kwamba mtaani wana hasira ,frustrations stress. Sijajua hii hali imesababishwa na nini.

Naomba mpate quick recovery.
 
Kiulinzi mkuu wa majeshi yupo juu maana akitekwa anaweza kutoa siri za kiulinzi za nchi. Kwa mkwanja Gavana anamzidi maana yeye kashikilia uchumi wa nchi!
 
Mkuu wa majeshi ni taasi kubwa kama ya rais!,na ndiyo maana nchi ikiingia kwenye machafuko ya kisiasa mkuu wa majeshi ana uwezo wa kuongoza nchi na jeshi lake na kutoa amri zinazotekelezeka!,hivyo si mtu wa mchezo mchezo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Majeshi ni mtu muhimu zaidi na analindwa kuliko Gavana. CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, yani majeshi yote hadi usalama wa taifa yapo chini yake. Gavana hamzidi chochote CDF

Sent from my iPhone using JamiiForums
Umeongeza chumvi, CDF ni mkuu wa majeshi ya ulinzi tu. Ukitaja usalama inamaanisha ni hadi jeshi la polisi na magereza, huko hahusiki. Na TISS haipo chini ya CDF, ipo chini ya DG wao. Rais pekee ndiyo hivyo vitu vyote vipo chini yake, ila si CDF
 
gavana ana taarifa nyeti za uchumi. Cdf ana taarifa nyeti za ulinzi na usalama wa nchi. Kwenye usalama, na taarifa za uchumi huingia.
 
unalinganisha cheo cha kijeshi na cheo cha kiraia?
 
Back
Top Bottom