Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Mkuu wa Mkoa ahojiwa na TAKUKURU
Na Jabir Idrissa, MwanaHALISI,
Jumatano, Agosti 5-11, 2009.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Leon Simbakalia amekiri kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).
MwanaHALISI imefahamishwa kwamba Simbakalia, Kanali mstaafu wa Jeshi la Ulinzi, alihojiwa na kamachero wa TAKUKURU kwa saa 5 mfululizo.
Mahojiano hayo yalifanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. Haikufahamika mkuu huyo aliyewahi kuwa mkurugenzi Mkuu wa NDC alihojiwa kwa tuhuma zipi.
Kwa karibu mwaka sasa kumekuwa na madai kuwa wakati Kanali Simbakalia akiwa Mkurugenzi Mkuu wa NDC kulitokea ubadhirifu wa dola 1.5 milioni (sawa na Sh 2 bilioni).
Imekuwa ikidaiwa kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya NDC haikuidhinisha matumizi ya fedha hizo kutoka benki ya Braclays Plc, London, Uingereza. Taarifa zinasema fedha hizo zilikuwa zizibe pengo la fedha za kutekeleza miradi ya Shirika ambayo haikuwa imepata fedha za serikali.
Fedha yote ya mradi uliokusudiwa ni dola 2.0 milioni. Sehemu ya fedha hizo, dola 500,000 ilitumika kukidhi gharama za utawala katika shirika, wakati kiasi kilichobaki, dola 1.5 milioni haikujulikana kilivyotumika.
Habari zaidi katika MwanaHALISI, Uk wa 3. WanaJF, mwenye soft copy ya full stoiry tunaomba aiweke hapa.