Mkuu wa Mkoa ahojiwa na TAKUKURU

Mkuu wa Mkoa ahojiwa na TAKUKURU

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239
Mkuu wa Mkoa ahojiwa na TAKUKURU

Na Jabir Idrissa, MwanaHALISI,
Jumatano, Agosti 5-11, 2009.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Leon Simbakalia amekiri kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

MwanaHALISI imefahamishwa kwamba Simbakalia, Kanali mstaafu wa Jeshi la Ulinzi, alihojiwa na kamachero wa TAKUKURU kwa saa 5 mfululizo.

Mahojiano hayo yalifanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. Haikufahamika mkuu huyo aliyewahi kuwa mkurugenzi Mkuu wa NDC alihojiwa kwa tuhuma zipi.

Kwa karibu mwaka sasa kumekuwa na madai kuwa wakati Kanali Simbakalia akiwa Mkurugenzi Mkuu wa NDC kulitokea ubadhirifu wa dola 1.5 milioni (sawa na Sh 2 bilioni).

Imekuwa ikidaiwa kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya NDC haikuidhinisha matumizi ya fedha hizo kutoka benki ya Braclays Plc, London, Uingereza. Taarifa zinasema fedha hizo zilikuwa zizibe pengo la fedha za kutekeleza miradi ya Shirika ambayo haikuwa imepata fedha za serikali.

Fedha yote ya mradi uliokusudiwa ni dola 2.0 milioni. Sehemu ya fedha hizo, dola 500,000 ilitumika kukidhi gharama za utawala katika shirika, wakati kiasi kilichobaki, dola 1.5 milioni haikujulikana kilivyotumika.

Habari zaidi katika MwanaHALISI, Uk wa 3. WanaJF, mwenye soft copy ya full stoiry tunaomba aiweke hapa.
 
Kumhoji?? au kumkamata..na kumfungulia mashtaka???

TAKURURU is a barking dog..it never bites!!!
 
Kumhoji?? au kumkamata..na kumfungulia mashtaka???

TAKURURU is a barking dog..it never bites!!!

Yeah... hata hiyo sifa ya ku-bark unawapa ya bure. nani ajali bark za TAKUKURU? Hapo ndiyo tayari wameshamaliza -- kuhoji, labda hadi mkuu wa kaya aseme 'kamata huyo!' -- kama vile kwa Prof Mahalu. Kwa maswahiba huishia hivyo hivyo tu -- kuhoji, basi.

Uhakika ni kwamba hatutasikia tena habari za Tuhuma dhidi ya huyo Kanali mwizi.
 
Sasa ivi nyie mnataka hao TAKUKURU wakamate watu bila kuwahoji/kuwasikiliza?? mi nadhani haya mambo yanatokea ktk nchi zenye aina flani ya udikteta na zisizofuata good governance....
 
barking and toothless...eti serikali kuipa meno kweli ilihitaji hilo?

Kama nipo correct the former anti corruption act (PCA) had only four corruption offences but the new act (PCCA) of 2007 inayo makosa (offences) 24 za corruption. Hayo ndo meno waliyopewa...na ukipewa meno sharti upewe na muda wa kuyazoea kama unataka kutafuna vizuri la sivyo utakuwa unajing'ata ulimi wako. LET'S GIVE THEM TIME PLZ!
 
Sasa ivi nyie mnataka hao TAKUKURU wakamate watu bila kuwahoji/kuwasikiliza?? mi nadhani haya mambo yanatokea ktk nchi zenye aina flani ya udikteta na zisizofuata good governance....

Kaka kuna mambo ya kufuata good governance na mengine can not......
mTU UWEZI KUWAIBIA WATANZANIA KIASI KIKUBWA CHA PESA AMBACHO NI JASHO LA WA-TZ, THEN UNATAKA TUFUATE SHERIA; HIYO NI HOPELESS KABISA..... Kama mambo yenyewe ndo hivi...KUPATA MAENDELEO KWA NCHI KAMA HII NI NDOTO.....
 
Takukuru wanakamata sana na kuwafukuzisha kazi MAHAKIMU WA MAHAKAMA ZA MWANZO.

Kwa hilo nawapongeza sana!>
 
Hatutaki tu mahakimu na madiwani au makatibu kata, bali na vigogo na mtu yeyote yule anayekwenda kinyume na sheria ya nchi.
 
Hatutaki tu mahakimu na madiwani au makatibu kata, bali na vigogo na mtu yeyote yule anayekwenda kinyume na sheria ya nchi.

TAKUKURU hawawezi kuwashitaki wakubwa mpaka kwa amri kutoka juu. Ingekuwa wanaweza, waombe ushahidi kutoka SFO na wamshitaki mzee wa Vijisenti na Dr Rashid. Au sivyo wawakabidhi kwa SFO wao wawashitaki.

Wamezoea kutuletea ngonjera tu za kusema wanamchunguza huyu, wanamchunguza yule, hakuna kinachokamilika -- kama vile sie ni watoto wadogo. EPA ni ujanjaujanja tu yaani kiini macho kukidhi presha ya wafadhili. Hakuna kitu pale.
 
Kwa hali na mazingira yaliyopo wahusika wa ufisadi wote wameshajifunza majibu ya kutoa, 'NILIZITOA ZIKATUMIKA KWENYE KAMPENI ZA UCHANGUZI 2005'. Siimekwisha? Takukuru wanamwambia wewe nenda kawatangazie tulikuchunguza ili kuwakeep busy, wakati tunaendelea na mambo mengine. Ndiyo chichi'em hiyo!
 
Mkuu wa Mkoa ahojiwa na TAKUKURU

Na Jabir Idrissa, MwanaHALISI,
Jumatano, Agosti 5-11, 2009.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Joseph Leon Simbakalia amekiri kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

MwanaHALISI imefahamishwa kwamba Simbakalia, Kanali mstaafu wa Jeshi la Ulinzi, alihojiwa na kamachero wa TAKUKURU kwa saa 5 mfululizo.

Mahojiano hayo yalifanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. Haikufahamika mkuu huyo aliyewahi kuwa mkurugenzi Mkuu wa NDC alihojiwa kwa tuhuma zipi.

Kwa karibu mwaka sasa kumekuwa na madai kuwa wakati Kanali Simbakalia akiwa Mkurugenzi Mkuu wa NDC kulitokea ubadhirifu wa dola 1.5 milioni (sawa na Sh 2 bilioni).

Imekuwa ikidaiwa kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya NDC haikuidhinisha matumizi ya fedha hizo kutoka benki ya Braclays Plc, London, Uingereza. Taarifa zinasema fedha hizo zilikuwa zizibe pengo la fedha za kutekeleza miradi ya Shirika ambayo haikuwa imepata fedha za serikali.

Fedha yote ya mradi uliokusudiwa ni dola 2.0 milioni. Sehemu ya fedha hizo, dola 500,000 ilitumika kukidhi gharama za utawala katika shirika, wakati kiasi kilichobaki, dola 1.5 milioni haikujulikana kilivyotumika.

Habari zaidi katika MwanaHALISI, Uk wa 3. WanaJF, mwenye soft copy ya full stoiry tunaomba aiweke hapa.

Ahhh! Hawa nao ndio zile zile tuu. Hivi samahanini kwenye hii thread, hivi Tanzania hatuna Shirika ama Idara inayokagua Vyeti FEKI na ningependa waanze kwa hao hao WAKUU WA MIKOA
 
mTU UWEZI KUWAIBIA WATANZANIA KIASI KIKUBWA CHA PESA AMBACHO NI JASHO LA WA-TZ, THEN UNATAKA TUFUATE SHERIA; HIYO NI HOPELESS KABISA..... Kama mambo yenyewe ndo hivi...KUPATA MAENDELEO KWA NCHI KAMA HII NI NDOTO.....[/QUOTE]

Tuwe tunatafakari kabla ya kujibu kitu jamani...sasa kama hautaki tufuate sheria tunazitunga za nini?tuvunje Bunge tumwachie Rais aongoze nchi anavyoona yeye.
Halafu kumbuka TAKUKURU ipo kwa mujibu wa sheria na inaongozwa kwa mujibu wa sheria, sasa kama unataka wasifuate sheria utakuwa umechoka kutafakari mambo kwa upana zaidi.
 
Back
Top Bottom