Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam asema bei ya saruji imeanza kushuka na baadhi ya wauzaji waliokuwa wakilangua wanahojiwa Polisi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam asema bei ya saruji imeanza kushuka na baadhi ya wauzaji waliokuwa wakilangua wanahojiwa Polisi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge amesema bei ya rejareja saruji imeanza kushuka na baadhi ya wauzaji waliokuwa wakilangua wanahojiwa Polisi.

Ameviagiza vyombo vya ulinzi kuendelea kuwakamata walanguzi wanaoendelea kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu.

Juzi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wakuu wote wa mikoa wafuatilie kubaini sababu za kupanda bei ya saruji wawe wamempa taarifa ifikapo keshokutwa Ijumaa.

Alitoa agizo hilo katika viwanja vya Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma baada ya Rais John Magufuli kumuapisha kuendelea na wadhifa huo. Kunenge alisema hakuna sababu ya bei kuendelea kuwa juu wakati kiwandani bei haijapanda.

“Serikali ya mkoa kamwe haiwezi kuwanyamazia watu hawa, ni lazima washughulikiwe kwa kila namna kwa kuwa huu ni wizi wanaoufanya kwa wananchi, ninasisitiza kwa wale wanaoendelea kuwaibia wananchi serikali itawashughulikia ipasavyo. Nimeambiwa kuwa wapo ambao walikamatwa kwa kulangua saruji na ninataka walanguzi kuacha mara moja kabla hawajachukuliwa hatua zaidi,” alisema Kunenge.

Meneja Mauzo Mwandamizi wa Kampuni ya Twiga Cement, Danford Semwenda alisema kampuni hiyo imepunguza kiwango cha saruji kwenda nchi jirani ya Rwanda kutoka tani 40,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 20,000.

Alisema kiwanda hicho kinaweza kuzalisha hadi tani 6,000 kwa siku hivyo kwa mwezi kinazalisha hadi tani 60,000.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alisema atatoa majibu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu atakapofanya uchunguzi na kupata majibu.

Akizungumza kwa simu jana, Byakanwa alisema kwa sasa yupo Dodoma na kwamba hawezi kutoa majibu sahihi kuhusiana na agizo hilo la Waziri Mkuu.

Hivi karibuni, Byakanwa alitembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote mkoani Mtwara na akawataka na kuwataka wasimamizi wa kiwanda hicho watangaze bei ya bidhaa hiyo.

“Nimewataka watangaze kwenye magazeti ili wananchi wote wajua kwamba bei yetu ya 'cement' inapaswa kuwa hii na akikuta imepanda asinunue atoe taarifa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya na pengine wakuu wa mikoa tuwatafute hao wafanyabiashara ambao wanataka kupata faida kinyume na utaratibu,” alisema Byakanwa.
 
Je, safari hii agizo la Majaliwa,litatekelezwa kweli,!?au along the way litapuuzwa Kama kawa wanavyofanyaga,lakini akija Magufuli akisema kidogo faster linatekelezwa tena kwa haraka sana!!
 
NAOMBA KUFAHAMU SARUJI INAPOPANDA BEI GHAFLA MAANA YAKE KUNA UPUNGUFU, JE WAKATI HUU INAPOPANDA BEI SIO WAKATI MZURI WA VIWANDA KUONGEZA UZALISHAJI ZAIDI ILI KUWACHOSHA HAO WALANGUZI WANAOFICHA BIDHAA HUSIKA? NASHAURI HAO WANAOFICHA WAACHWE WAFICHE NA VIWANDA VICHAPE TU KAZI TUONE NINI KINAKUJA KUTOKEA akili zangu ni za kimagufuli zaidi kazi kazi tu
 
Kwa approach Kama hizi tutarudi kule kule kwenye sukari
 
Serikali itupe Watanzania orodha ya bidhaa zote na Bei zake elekezi. Kuanzia bei ya dagaa kwa fungu hadi bei ya Passo.

Hii nchi ni ya ajabu kabisa
Ninao Uhakika Kuna watu humu wamenunulia yani wanatumika ikiwemo wewe......Nakusikitikia sana
 
Mkoa wa Dar es Salaam unahitaji Mkuu wa Mkoa mwenye Moyo kama wa 'Mwendawazimu' vile, ila Kwangu Mimi huyu wala sioni analolifanya hasa.
 
Masuala ya uchumi hayajawahi kutatuliwa kwa kutumia polisi na matamko.Kama gharama za maisha kama vile mafuta,bei za vyakula,mishahara,gharama za usafirishaji,vipuri vya service,umeme,e.t.c zimepanda hakuna namna ya kuuza hiyo saruji bei ya chini.

Wanajidanganya tu.Suluhisho pekee ni kudeal na uchumi mzima wa nchi katika aggregation level.Wanachofanya sasa hivi ni sawa na kuzuia mto huku chini badala ya kwenda kuziba kwenye chanzo!
 
atleast g

SASA HII NDIYO INTELLEGENCE #behaiuorist, KILA MAHALA NI KUTUMIA POLISI TU VIPO VITU HAVIITAJI POLISI KABISA hapa ni hesabu kidogo tu mkutano wa siku moja na wazalishaji tatizo linakwisha
 
NAOMBA KUFAHAMU SARUJI INAPOPANDA BEI GHAFLA MAANA YAKE KUNA UPUNGUFU, JE WAKATI HUU INAPOPANDA BEI SIO WAKATI MZURI WA VIWANDA KUONGEZA UZALISHAJI ZAIDI ILI KUWACHOSHA HAO WALANGUZI WANAOFICHA BIDHAA HUSIKA? NASHAURI HAO WANAOFICHA WAACHWE WAFICHE NA VIWANDA VICHAPE TU KAZI TUONE NINI KINAKUJA KUTOKEA akili zangu ni za kimagufuli zaidi kazi kazi tu
Tatizo Walanguzi lazima wale Mchongo na watu wa Production,ili uzalishwaji ubanwe kidogo,ili kuleta high price kwenye Market!!
 
Sukari ilikua inafichwa na wafanya biashara.
kama wakificha siment inaweza kukaa muda mrefu bila kuharibika?
Ni utunzaji tu mkuu... unafikiri hata kwa hiyo bei iliyopanda ni wangap waneweza kumudu kununua
 
Bora wakamatwe.cement utauzaje elfu 20 kwa dar wakati kiwanda hakijapandisha Bei ya cement?.
Kisa haipatikani ndo upandishe Bei?.
Hizi approach za kukamata zitafanya cement ipotee kabisa sokon rejea ishu ya sukari
 
Mzee hao waliokamatwa Ni wale waliokuwa wanauza cement kwa Bei ya juuu.kiufupi cement haijapanda Bei kiwandani.hapa nawatetea POLISI.
Kutopatikana kwa cement isiwe sababu ya kupandisha Bei kiholela.
Masuala ya uchumi hayajawahi kutatuliwa kwa kutumia polisi na matamko.Kama gharama za maisha kama vile mafuta,bei za vyakula,mishahara,gharama za usafirishaji,vipuri vya service,umeme,e.t.c zimepanda hakuna namna ya kuuza hiyo saruji bei ya chini.

Wanajidanganya tu.Suluhisho pekee ni kudeal na uchumi mzima wa nchi katika aggregation level.Wanachofanya sasa hivi ni sawa na kuzuia mto huku chini badala ya kwenda kuziba kwenye chanzo!
 
Mzee hao waliokamatwa Ni wale waliokuwa wanauza cement kwa Bei ya juuu.kiufupi cement haijapanda Bei kiwandani.hapa nawatetea POLISI.
Kutopatikana kwa cement isiwe sababu ya kupandisha Bei kiholela.
Huwezi ukaamka asubuhi ukaanza kuuza kitu kwa bei ya juu from nowhere!
 
Back
Top Bottom