Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam asema bei ya saruji imeanza kushuka na baadhi ya wauzaji waliokuwa wakilangua wanahojiwa Polisi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam asema bei ya saruji imeanza kushuka na baadhi ya wauzaji waliokuwa wakilangua wanahojiwa Polisi

Tatizo sio kuamka asubuhi na kupandisha Bei.tatizo viwanda havijapandisha Bei ya cement.mimi mwenyewe nauza hardware lakini siwezi kuwatetea hao jamaa waliopandisha Bei ya cement.maana cement haijapanda wao wamepandisha Bei ya cement kwa kigezo kipi?
kutopatikana kwa bidhaa sio sababu ya kupandisha Bei hapo Wana makosa.
Na cement haijapanda Bei TATIZO HAIPATIKANI.
Huwezi ukaamka asubuhi ukaanza kuuza kitu kwa bei ya juu from nowhere!
 
Soda bei elekezi ni 500 lakini inauzwa 700, 800, mpka 1000.
Bia hali kadhalika.
Sasa hii cement ni bidhaa peke yake yenye bei elekezi? Mafuta yanapanda maanake bei ya usafiri inapanda pia.

Sent from Hell
 
Tatizo sio kuamka asubuhi na kupandisha Bei.tatizo viwanda havijapandisha Bei ya cement.mimi mwenyewe nauza hardware lakini siwezi kuwatetea hao jamaa waliopandisha Bei ya cement.maana cement haijapanda wao wamepandisha Bei ya cement kwa kigezo kipi?
kutopatikana kwa bidhaa sio sababu ya kupandisha Bei hapo Wana makosa.
Na cement haijapanda Bei TATIZO HAIPATIKANI.
Kwa nini haipatikani?
 
Acha iendelee kupanda, kujenga si maendeleo ya vitu!
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge amesema bei ya rejareja saruji imeanza kushuka na baadhi ya wauzaji waliokuwa wakilangua wanahojiwa Polisi.

Ameviagiza vyombo vya ulinzi kuendelea kuwakamata walanguzi wanaoendelea kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu.

Juzi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliagiza wakuu wote wa mikoa wafuatilie kubaini sababu za kupanda bei ya saruji wawe wamempa taarifa ifikapo keshokutwa Ijumaa.

Alitoa agizo hilo katika viwanja vya Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma baada ya Rais John Magufuli kumuapisha kuendelea na wadhifa huo. Kunenge alisema hakuna sababu ya bei kuendelea kuwa juu wakati kiwandani bei haijapanda.

“Serikali ya mkoa kamwe haiwezi kuwanyamazia watu hawa, ni lazima washughulikiwe kwa kila namna kwa kuwa huu ni wizi wanaoufanya kwa wananchi, ninasisitiza kwa wale wanaoendelea kuwaibia wananchi serikali itawashughulikia ipasavyo. Nimeambiwa kuwa wapo ambao walikamatwa kwa kulangua saruji na ninataka walanguzi kuacha mara moja kabla hawajachukuliwa hatua zaidi,” alisema Kunenge.

Meneja Mauzo Mwandamizi wa Kampuni ya Twiga Cement, Danford Semwenda alisema kampuni hiyo imepunguza kiwango cha saruji kwenda nchi jirani ya Rwanda kutoka tani 40,000 kwa mwaka hadi kufikia tani 20,000.

Alisema kiwanda hicho kinaweza kuzalisha hadi tani 6,000 kwa siku hivyo kwa mwezi kinazalisha hadi tani 60,000.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alisema atatoa majibu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu atakapofanya uchunguzi na kupata majibu.

Akizungumza kwa simu jana, Byakanwa alisema kwa sasa yupo Dodoma na kwamba hawezi kutoa majibu sahihi kuhusiana na agizo hilo la Waziri Mkuu.

Hivi karibuni, Byakanwa alitembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Dangote mkoani Mtwara na akawataka na kuwataka wasimamizi wa kiwanda hicho watangaze bei ya bidhaa hiyo.

“Nimewataka watangaze kwenye magazeti ili wananchi wote wajua kwamba bei yetu ya 'cement' inapaswa kuwa hii na akikuta imepanda asinunue atoe taarifa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya na pengine wakuu wa mikoa tuwatafute hao wafanyabiashara ambao wanataka kupata faida kinyume na utaratibu,” alisema Byakanwa.

Price is controlled by demand and supply! Jinamizi la sukari linaamka, na huwa linaamka week ya kwanza ya utawala!
 
serikali kuachia uchumi uendeshwe na private ni shiiiiiiida zile hadithi za 666 kumbe inawezekana kutokea ,ili upate kitu chochote sharti pigwa chapa


1605702586949.png
 
Solution rahisi ya simenti kupanda bei ni kuzalisha mara dufu,,
Material yapo,umeme upo,,tabu iko wapi?
 
Hahaha yani hata wasiohitaji cement wanasema imepanda bei.

Muwe mnajadili na unga wa ugali yani dona, sembe, bila kusahau mchele na maharage haya ndiyo mahitaji yetu sote.
 
Back
Top Bottom