Mkuu wa Mkoa wa Dar ni nini kinakwamisha ukarabati wa miundombinu ya maji taka hapa Canossa School?

Mkuu wa Mkoa wa Dar ni nini kinakwamisha ukarabati wa miundombinu ya maji taka hapa Canossa School?

The Saver

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2014
Posts
202
Reaction score
651
Kwako Mkuu wa Mkoa, Kunenge ni masikitiko makubwa wewe kama Mkuu wa Mkoa umekaa kimya na najua unachokiona hapa kimekufikia.

Je, wewe Mkuu wa Mkoa nyumbani kwako unakaa karibu na dampo la takataka?

Je, watoto wako wanasomea shule na wanavuta harufu na takataka za dampo?

Mkuu wangu unajua na taarifa zimekufikia mlifunga barabara ya kwenda Canossa Primary sababu ya kuboresha miundombinu ya maji taka ya Tegeta sokoni lakini ni mwaka sasa kazi hii haijaisha na wewe upo umekaa ofisini unapata kiyoyozi.

Sasa mkuu kwa muda sasa sehemu anaposomea watoto wetu ndio seheme ya kumwaga taka tena taka zinamwagwa getini, pia karibu na madarasa ya kusomea watoto wetu.

Je, wewe mkuu wa mkoa kwanini unataka kuua afya za watoto wetu?

Serikali ya Mtaa, Diwani, Mkuu wa Wilaya wote kimya kama hawajui kuwa watoto wanateseka.

Hii hoja nimeleta kwako maana hii ipo ndani ya mkoa wako na najua hii imekufikia.



IMG_20210426_084548.jpg

IMG_20210426_084530.jpg

IMG_20210426_084517.jpg
 
Ila binadamu Bana kwakuwa hao watoto wako wanasoma hapo basi unaona kira kitu kibaya. Acha kudeka, kupata kihera kidogo Tu unaona watoto wako watapata maradhi. Kule kijijini kwenu yaani Kwa Bibi yao maji ya kunywa yameshabadirika rangi tayari, mkuu WA mkoa ni mkubwa Sana Acha kuchafua taswila yake Kwa hicho kijihada chako cha hapo canosa kwani ukujua kwamba shule iko uchochoroni?? Anza na mjumbe Kwanza ndio kazi zao hizo😂😂😂😂😂
 
Ila binadamu Bana ......kwakuwa hao watoto wako wanasoma hapo basi unaona kira kitu kibaya......Acha kudeka......kupata kihera kidogo Tu unaona watoto wako watapata maradhi ....Kule kijijini kwenu yaani Kwa Bibi yao maji ya kunywa yameshabadirika rangi tayari.......mkuu WA mkoa ni mkubwa Sana Acha kuchafua taswila yake Kwa hicho kijihada chako cha hapo canosa kwani ukujua kwamba shule iko uchochoroni?? Anza na mjumbe Kwanza ndio kazi zao hizo😂😂😂😂😂
Asante ila najua wewe Huna mtoto hujui afya za watoto.

Hapa hatutaelewana.
 
Nadhani hoja hii inatakiwa ielekezwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa. Huyo ndiye aliyepewa rasilimali watu, fedha na vifaa. Huyu Mkuu wa Mkoa ni msimamizi tu.
 
Nadhani hoja hii inatakiwa ielekezwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa. Huyo ndiye aliyepewa rasilimali watu, fedha na vifaa. Huyu Mkuu wa Mkoa ni msimamizi tu.
Kwa jinsi ilivyo nahisi mkurugenzi wa manispaa Ana taarifa maana hii imekuwa kero ya muda mrefu

Sasahivi wamebadirisha utaratibu wa kumwaga taka zamani walikuwa wanamwaga taka chini harufu kama zote na watoto wapo madarasani wanasoma
 
Back
Top Bottom