JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Uamuzi wa Shigela unakuja kufuatia kutoridhishwa na majibu ya maofisa hao wa GGML juu ya malipo ya malimbikizo ya fedha za Uwajibikaji wa Makampuni kwa Jamii (CSR) mwaka 2024, Tsh. Bilioni tisa.
Shigella alisema fedha za CSR ni pesa ya wananchi na siyo pesa za mtumishi wa GGML na haitolewi kama hisani bali ipo kwa mjibu wa sheria na kanuni za madini na hivo GGML haipaswi kuleta mzaha katika utekelezaji wa CSR.
Mbunge wa Jimbo la Chato, Dk Medard Kalemani alipongeza uamuzi wa mkuu wa mkoa na kueleza kuwa kanuni ya 140 ya sheria za madini inatambua CSR inatekelezwa kwa mjibu wa sheria na siyo hisani.