Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Gaguti hizi chuki zako uwe pia unazionyesha hadi kwa Yanga SC na si Simba SC pekee

International Pumba
 
Labda leo nikukumbushe tu kuwa ' Upuuzi ' huu huu ambao leo unaufanya alianza Kuufanya mwana Yanga SC mwenzio Mbunge Mwigulu Nchemba alipokua Waziri na ni hapa hapa ' tulimuonya ' kuwa anachokifanya ' Kitamgharimu ' nafasi yake ya Uwaziri ambapo tulimshtakia hapa hapa JamiiForums kwa Mheshimiwa Rais na hatimaye ' akaliwa Kichwa ' na sasa anajutia.

Najua Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime ni Yanga SC Kindakindaki na kwamba kila akicheza na Simba SC ( Kupitia Kagera Sugar ) yake huwa anakuwa na ' Hirizi ' ambayo huiweka sana katika Mfuko wake wa Kushoto wa Suruali yake hivyo mwambie kuwa Siku ya Alhamisi aivae tena na Simba SC tusije Kulaumiwa kama ' Akifa ' pale Uwanjani.

[/QUOTE]

😀😀 aisee utakoma na simba yako................
 
Wacha kulia lia ila wahimize wachezaji wa timu yako wakaze buti tu na hakuna uchawi mwingine wala visingizio.
 
Raisi pekee Tanzania aliyejulikana timu gani ni Kikwete hadi kadi anayo..hii ya Magufuli ni kujitapatapa tu..hana hata kadi...Kagera anakufunga hadi Taifa ..aarrggghh kwa nini nimechangia mechi za mchangani
 
Kakojoe ulale//hovyo kabisa
 
Kuhusu Simba kuwa mahiri wa kuroga na kutandaza kandanda, hilo halina mjadala. Simba wanakuroga, na wanakupigia soka hadi unatoka na possession zako za 30%. Hata Yanga wanajua, mara ya mwisho kuifunga Simba ni miaka mitatu iliyopita. Yanga hawajapata ushindi mbele ya Simba, na ndio maana wanategemea walau Kagera awasaidie kuifunga Simba. Safari hii watu kibao watapigwa mkono ligi ya Bara
 
Kachezeni mpira nyie Mikia FC.......
 
Unamuonea bure mkuu wa mkoa wetu, mbona tunawafunga hata mkiwa huko kwenu dar. Tulipo wafunga kipindi kile mlienda hadi fifa mkidai malinzi kawahujumu, tukatoboa tundu mbele ya mheshimiwa, mwaka jana tuka wa zantel kote kote. Acheni visingizio.
 
Hili jamaa jinga kweli unataka kusema Mwigulu alitumbuliwa baada ya wewe kumshtakia rais hapa jf kwamba yule ni mnazi wa Yanga?
 
Nafikiri sio busara kuanza kuwapa wachezaji uoga usio na sababu mara sijui mkuu wa mkoa, mara hirizi mara mexime. Hayo yote yatawajengea hofu wachezaji wa Simba. Kama kweli wewe ni shabiki wa Simba nilitegemea kuwa uwape moyo wachezaji na viongozi kuwa ni kweli Kagera Sugar ni mwiba kwa Simba lakini safari hii mnakwenda kubadilisha historia ukizingatia mmefanya usajili wa mabilioni. Tafuteni hata mtu wa saikolojia awasaidie kuwatoa kwenye huu mzimu wa kushindwa na Kagera lakini sio hayo mawazo ya kizamani na kutaka kuwapa watu lawama wasizostahili. Kwani mkuu wa mkoa kuhamasisha kafanya kosa gani? Je, yeye anaingia uwanjani kuongeza idadi ya wachezaji wawe 13? Hivi kwa mawazo kama haya ndio tulikuwa tunategemea kuwatoa UD Songo halafu twende makundi, robo fainali halafu nusu fainali CL?

Nina hakika Simba itaishinda tu Kagera iwapo itaachana na mawazo potofu na kuamua kucheza mpira kwani ina kikosi bora na haihitajiki mambo mengine nje ya uwanja wa mpira kuweza kupata ushindi.
 
Na wakiendako JKT Ruvu je? Huwa inakuwaje?
 
Mwaka huu muwatigotigo ndiyo size yao
Unamuonea bure mkuu wa mkoa wetu, mbona tunawafunga hata mkiwa huko kwenu dar. Tulipo wafunga kipindi kile mlienda hadi fifa mkidai malinzi kawahujumu, tukatoboa tundu mbele ya mheshimiwa, mwaka jana tuka wa zantel kote kote. Acheni visingizio.
 
Mwache RC afanye kazi yake,ulikuwa humuoni Amosi Makala alivyokuwa mbeya,Yanga ikienda alikuwa anahaha ili ifungwe? Huyu RC wa Kagera ni mzalendo🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…