Mkuu wa Mkoa wa Morogoro apiga marufuku Walimu kuwekwa ndani

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro apiga marufuku Walimu kuwekwa ndani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008

RC apiga marufuku walimu kuwekwa ndani​

Martine Shigela alitoa agizo hilo wakati wa akifungua kikao cha wadau wa elimu wa mkoa wa Morogoro katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM) kilicholenga kutathmini masuala ya sekta hiyo.
Kikao kazi hicho cha wadau wa sekta ya elimu mkoa kilibeba kaulimbiu isemayo “Ushirikishwaji wa Wadau kwa Elimu Bora”

Alisema licha ya kwamba mambo hayo hayajatokea ndani ya mkoa, lakini ikitokea mwalimu amekiuka mambo fulani ambayo si ya kijinai, ni marufuku kumweka ndani. “RPC (Kamanda wa Polisi wa Mkoa) upo hapa. Sipendezewi na sitaki kuona walimu wanawekwa ndani. Akiwekwa ndani kesho yake unaingia darasani kufundisha. Ziko njia nyingi za kumwonya, ninataka jambo hili lisiwapo mkoani hapa na kama lilishatokea, lisijirudie tena,” alionya.

Mkuu wa mkoa alisema endapo kuna mwalimu hatimizi wajibu wake vizuri na hajafanya jambo lolote la kijinai, hakuna sababu ya kumweka ndani.

Aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote ndani ya mkoa wakishirikiana na wadhibiti ubora wa elimu kuhakikisha shule zote ambazo hazijasajiliwa na serikali kuharakisha kuziwezesha kupata sifa za kusajiliwa.
Mkuu wa mkoa alisema hatua hiyo itapunguza mrundikano wa wanafunzi katika baadhi ya shule zilizoko kwenye halmashauri.

Katika hatua nyingine, Shigela aliwataka wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu wa shule za msingi kuwa wabunifu katika shule zao kulingana na mazingira yao.

Shigela aliwataka wakishirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali za vijiji na kata katika kuziendeleza shule zao kwa kuwa jambo hilo litaleta hamasa ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Naye Ofisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro, Germana Mung'aho, alisema wanafunzi 210 wa shule za msingi na sekondari wamerudi kuendelea na masomo katika mfumo rasmi baada ya kuacha kwa sababu mbalimbali zikiwamo mimba na utoro sugu.

Mung'aho alisema kupitia wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, mkoa umetekeleza kwa kiwango kikubwa agizo la Rais la wanafunzi waliocha shule kwa sababu mbalimbali kurudi shuleni katika mfumo rasmi.

Alisema kati ya walionufaika kurudi kuendelea na masomo wako wasichana 10 waliokuwa wamepata mimba wakiwa wanasoma shule za sekondari za halmashauri ndani ya mkoa.

Kwa upande wa shule za msingi, alisema wanafunzi 200 wamerudi shuleni na kati ya hao 98 ni wasichana waliacha kutokana na sababu nyingine na wavulana wakiwa 69.

Mung'aho alisema katika idadi hiyo pia kuna wanafunzi 12 wa kike waliokuwa watoro sugu na wavulana 21 ambao nao wamerudi kuendelea na masomo.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom