Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza imesikitishwa na taarifa zilizoenezwa na baadhi ya watu kuwa mkuu wa mkoa Mhe Said Mtanda amevamia mazoezi ya Simba akiwa na polisi na kuwashikili meneja wa timu na kocha msaidizi, Taarifa hizi si sahihi
Ukweli ni kuwa mkuu wa mkoa alipokea simu kutoka kwa maafisa wa Jiji la Mwanza kuwa walikuwa wamefungiwa uwanjani CCM kirumba na wanaomba msaada wa Polisi kwenda kuwatoa wakiwa hapo uwanjani kwani walinzi wa Simba waliwazuia kwenye vyumba
Mkuu wa mkoa alimuelekeza kamanda kwenda kuangalia usalama kwenye eneo la tukio lakini na yeye aliamua kwenda kuhakiki ili polisi wasije kuleta taharuki
Alifika kirumba na hakuingia uwanjani alisimama nje ya uwanja na polisi walifanikiwa kuwatoa vijana waliokuwa wamezuiliwa ndani na kwenda kuwahoji, na walifanikiwa kumchukua mlinzi mmoja wa simba aliyefanya tukio hilo kwa mahojiano aidha kwa tuhuma za kuvunja mlango na vioo vya uwanja.
Soma Pia: Vurugu kali zimezuka Uwanja wa CCM Kirumba wakati Simba SC ikifanya mazoezi kuelekea mechi na Pamba Jiji hapo kesho
Kama mwenyekiti wa kamati ya usalama anawajibika kusimamia usalama wa wananchi wote wakiwemo hao waliozuiliwa na kufanyiwa shambulio
Hakuna kocha wala kiongozi aliyekamatwa aidha hakuna uvamizi wowote uliofanywa na polisi wala mkuu wa mkoa
Aliyekamatwa alikamatwa baada ya kwisha kwa mazoezi hakukuwa na kuingilia kwa mazoezi ya Simba kwa namna yeyote.
Shabiki wa timu yoyote akifanya makosa atachukuliwa hatua za kisheria na polisi wanawajibika kusimamia hilo.
Mkuu wa mkoa wa mwanza anawataka wapenzi wa soka kuimarisha amani na usalama katika viwanja vya michezo