Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Saidi Mtanda, ameisihi jamii ya Kitanzania kuwaepuka watu aliowataja kufanya uchochezi wenye lengo la kuvuruga amani katika taifa, akisema ikiwa jamii na viongozi wataruhusu hayo, itasababisha madhara ambayo ni vigumu kuyashughulikia. Mtanda ameeleza hayo katika kongamano la amani la viongozi wa dini mbalimbali lililofanyika mkoani Mwanza leo Oktoba 20, 2025, ambapo pia alihudhuria kama mgeni rasmi.
“Kipindi kama hiki wapo watu ambao wanaandaa chokochoko ili kuhatarisha usalama, halafu kuondoa amani yetu, pia wapo wanaoweza kutumika kupitia dini, kupitia asasi mbalimbali hata ndani ya serikali, Rais anatutaka tusikubali kuchokozeka. Tusikubali kutoa kauli sisi viongozi wa dini hasa zile kauli ambazo zinaweza kuleta madhara baadaye, maneno ni kama risasi- ikishatoka haiwezi kurudi ilikotoka” ameeleza Mtanda.
Amewataka viongozi wa dini kuwa wavumilivu na wenye ustahimilivu, hasa wanapoona yapo mambo hayaendi katika usawa wake. Amesema serikali ipo tayari kukosolewa lakini katika ustaarabu akisema ukosoaji usiozingatia utaratibu ni uchochezi. “Mkikosoana kwa chuki, mkikosoana katika misingi ya jinsia, tukakosoana katika misingi ya imani zetu, ukosoaji huo unaweza ukatafsiriwa kwamba ni uchochezi na unalengo la kuwagawa watu” amesema Mtanda. Kongamano hilo limeandaliwa na Kamati ya amani ya viongozi wa dini mbalimbali mkoa wa Mwanza, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Said Mtanda, likiwa na mada isemayo “Uchaguzi ni Muda wa Maamuzi, Tushiriki Sote. Tudumishe Amani na Mshikamano kwa Maendeleo ya Taifa”