LAMBULAKATA
New Member
- May 12, 2020
- 0
- 8
NA: ALLY KATALAMBULA
Kwa sentensi ndefu na wino uliokolezwa kwa maandishi makubwa na madogo, mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Mh: Chritina Mndeme, SIYO RAIA WA TANZANANIA na kwa miaka mitano ya JPM yeye ndio ‘Man Of The Match’
Sauti imetosha? Au niongeze kidogo?
Siku za nyuma niliwahi kuandika Makala moja kwenye gazeti moja mashuhuri tu hapa nchini na hata kwenye majukwaa mbalimbali ya habari kama vile JamiiForums, Makala iliyokuwa na kichwa kilichosema:
MH: MNDEME NI KOBE ANAYESHINDA MBIO ZA MARATHONI
Maswali na maoni yakawa mengi. Wengine wakaponda kwa kuwa tu eti kiongozi huyu yupo chini ya chama talawa (CCM) Chama ambacho ni tofauti na chama chake.
Ajabu!
Hili la chama likatosha kuwa kibali cha wao kupatwa na maradhi ya upofu na uziwi, dhidi ya uadilifu wa mama huyu, mama ambaye upole, huruma, na uchapakazi ni sehemu tu ya tunu adhimu alizobarikiwa.
Sitaki kuwa mnafiki, kusubiri hadi mtu afe ndio nianze kumpamba kwenye mitandao kwa makala na tungo ndefu zenye ngano na vigano, mbwembwe na mashairi kibao. Kwangu tabia hizo sina, zilikwisha niacha mkavu zikapitia dirishani na kutokomea kusikojulikana.
Ukiniamsha usiku wa manane, ukaniuliza, “Bwana Ally Katalambula, ni teuzi gani bora ya JPM unavutiwa nayo tangu jemedari huyo aingie madarakani?”
Bila kigugumizi na kwa sauti ya juu, nitakwambia ni uteuzi ule wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma…Mh Chritina Mndeme.
Ukiniuliza tena kwa nini? Nitakujibu:
Tabia, mienendo, hulka, silka, kareba na aina ya maisha anayoishi RC Mndeme ndio sababu kwa nini ninavutiwa na ninampenda sana huyu Bi: Mkubwa!
Tabia za maisha ya RC Mndeme huwa zinanifanya niwaze mbali na kufikiria pengine huyu muheshimiwa siyo raia wa Tanzania. Kwa nini tabia zake zinatofautiana na Watanzania wengi.
Twende taratibu utanielewa.
Kiasili, RC Mndeme ni Mtanzania halisi, tena nijuavyo ni mnyamwezi wa Igalula huko vijijini. Lakini kutokana na namna anavyoishi na kuendesha maisha yake, mimi binafsi nimelazimika kuibua swali hilo zito, kwamba mbona huyu mama hafanani na tabia za Watanzania wengi? Au ana asilia ya nchi za nje?
Usiwe na haraka twende polepole utanielewa
Ongea yake ya upole, nywele zake nyeusi tii, mashavu yake, macho, na midomo vyote kwa ujumla ukiviona, haiba hiyo inahitimisha taswira ya kuwa, sio tu ni mtumishi bora wa umma, lakini pia ni mama wa familia bora.
Tuachane na hayo, turudi sasa kwenye hoja ya msingi:
Watanzania tulio wengi, tumekuwa wanafiki mno, hata kama mtu umemkosea, bado atakuchekea hadi jino la mwisho. Ukimpa kisogo anakusema vibaya mno. Lakini RC Mndeme akichukia, lazima akuoneshe kwamba amechukia.
Huyu kiongozi licha ya kwamba ni mwanamke lakini hapendi majungu na umbea, mambo yake yamenyooka wima, yanii kama mzungu f’lani hivi. Sio kiongozi wa maneno maneno. Muda wote yeye anapenda mzungumze kuhusu kazi tu.
Bahati mbaya masikini ya Mungu, viongozi wa namna hii kwa nchi yangu hii ya Tanzania, ni aghalabu sana kukuta vyombo vya habari vimewapa nafasi kwenye kurasa za vyombo vyao vya habari.
Ngoja nikunong’oneze kitu nje ya mada kidogo. Kwenye uandishi wa habari kuna ‘theory’ inayoitwa ‘Media Agenda Setting’ ambayo kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi inasema:
“Media inachagua watu wafikirie nini? Lini wafikirie jambo fulani? na vipi wafikirie? na kwa nini wafikirie jambo hilo?”
Kwa bahati mbaya kwa taifa langu hili pendwa, vyombo vya habari havina ‘Agenda setting’ inadaiwa sasa hivi ‘Agenda setting’ imekuwa ikibuniwa na baadhi ya wanasiasa wa kada na itikadi mbalimbali. Utakuta kuna kundi fulani la viongozi au wanasiasa, mwezi mzima vyombo vya habari vinawaongelea wao tu.
Kila kukicha wanasiasa na viongozi wanabuni kitu gani kitakachowafanya majina yao yawe mbele ya magazeti ya kila siku. Wakati huo viongozi sampuli ya Mh: Mndeme, ambao wengi wao ndio wapiganaji na wabeba maono ya rais Magufuli, wanashindwa kabisa kutambulika mbele ya umma.
Ukiwa na RC Mndeme, zungumzia maisha na maendeleo! Ukianza kuzungumzia watu na maisha yao binafsi, bila kuchelewa atakuambia, ‘mwanangu sina muda wa kujadili watu, nina mambo mengi ya kuwatumikia wananchi wangu wa Ruvuma’
Huyu muheshimiwa ni mama fulani hivi mnyenyekevu. Mtiifu na muungwana sana! Tofuati na viongozi wengine au watu waliofanikiwa kimaisha, ukimpigia simu ya mkononi, muda wowote (kasoro usiku) anapokea na kukusikiliza kwa makini.
Ni mtu wa vitendo. Kila kitu kizuri ukimwambia atakuitikia, ‘sawa’.
Akiona udhaifu na mapungufu kwako, anakuita na kukueleza hapohapo. Baada ya hapo maisha mengine yanasonga. Lakini Watazania wengi, akiona udhaifu kwako, kabla ya kukuambia anaanza kwanza kukuundia vikao vya maseng’enyo! Atakusema kwa kila neno baya ndipo anakufuata! Unafiki na uzandiki mkubwa Rc Mndeme ni tofauti. Anakueleza na kuishia hapohapo!
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, ana tabia za tofauti na Watanzania wengi. Ndiyo maana huwa nafikia mahali ninajiuliza na kuhitimisha labda siyo raia wa TANZANIA, ingawa ninajua ni mwenyeji wa Igalula huko Tabora. Kwa hiyo ni Mtanzania na raia halisi lakini tabia zake zinatofautiana na Watanzania wengi, ndiyo maana nikawaza, labda kiongozi huyu ‘SIYO RAIA WA TANZANIA!’
NB: Andiko lijalo nitakueleza nilivyomuibukia nyumbani kwake na kumkuta anakula ugali na mlenda, mama huyu.