Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi, ameonya dhidi ya watu wanaodhani kuwa wana nguvu zaidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza wakati wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Stephen Wasira, Kihongosi alisisitiza kuwa CCM ndicho chenye mamlaka katika mkoa huo.
"Asisimame mtu yeyote mahali popote ndani ya mkoa huu akaamini ana nguvu kuliko Chama Cha Mapinduzi, anajidanganya. Hatutakubali tabia ya kuzusha fitina, majungu, chuki, na watu kutafuta sifa badala ya kuimarisha chama," alisema.
Aidha, alikanusha madai ya mafanikio binafsi, akisisitiza kuwa miradi yote ya maendeleo inatekelezwa kwa fedha za serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
"Haiwezekani mtu asimame aseme 'mimi nimefanya.' Umefanya kwa hela gani? Hela imeletwa na serikali chini ya Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan," aliongeza Kihongosi.