Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Dkt. Philemon Sengati, ameagiza kushushwa vyeo kwa walimu wakuu wa shule ambazo zimekuwa zikifanya vibaya katika matokeo ya mitihani.
Alitoa kauli wilayani Urambo wakati wa mkutano na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo kwenye ziara ya kikazi.
Dkt. Sengai alisema walimu wakuu wasiokuwa wabunifu wa kuziwezesha shule zao kupandisha ufaulu wa wananfunzi ili waweze kuondokana na daraja sifuri, la nne na tatu hafai kuendelea na nafasi zao.
Alisema ni vema wakaondolewa na nafasi zao kukabidhiwa walimu ambao wako tayari kufanyakazi kwa kujituma na uzalendo ili waweze kuchochea ufaulu katika shule zao na mkoa kwa ujumla.
“Tunataka walimu wale ambao wako ‘committed’ na willingness na wanafanyakazi kwa uzalendo mkubwa, hao ndio tuendelee kuwafanya kuwa wakuu wa shule ili waendelee kuwa injini ya ufaulu wa shule zetu,” alisema.
Alisema walimu lazima wasaidie kusimamia maadili na kuwahimiza wanafunzi kusoma kwa ushirikiano na kuwawezesha kuongeza ufaulu ili wautangaze kwa kushika nafasi za juu.
Alisema moja ya kipaumbele cha uongozi wake ni elimu kwa kuwa ndio itasaidia kuwapaisha wakazi wa Mkoa wa Tabora kiuchumi na maendeleo mbalimbali.
IPPMedia