Mkuu wa Shule adaiwa kuhujumu wanafunzi wa Kiislamu Bagamoyo

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
18,887
Reaction score
7,673
MKUU wa Shule sekondari ya Bagamoyo, anadaiwa kupandikiza chuki za kidini huku akiwapachika ‘ugaidi’ wanafunzi

Waislamu wanaoswali swala tano.

Mkuu huyo anadaiwa kuwaita wanafunzi hao kuwa ni Al Qaida na Al Shabab huku akijumuika na wanafunzi Wakristo

akiwataka wakae mbali na ‘magaidi’ hao. Kutokana na chuki iliyojengeka shuleni hapo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani

ameamua kufunga shule hiyo huku hatma ya Mkuu huyo wa Shule ya Sekondari ya Bagamoyo, Bw. Bonus Ndimbo,

akiiacha mikononi mwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Hajjat Mwantum Mahiza, amelazimika kufunga Shule hiyo mapema wiki hii, baada ya kuwepo

mgogoro wa Kidini Shuleni hapo kwa muda mrefu jambo linaloashiria hali ya hatari. Akiongea na mwandishi wa habari

hizi, Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani, baada ya kutangaza kuifunga Shule hiyo, alisema suala hilo amelikabidhi kwa

Wizara husika (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi) kwa ajili ya uchunguzi zaidi juu ya mgogoro huo na hatma yake.

Hajjat Mahiza, alisema jukum lake akiwa kama Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa, ni kuhakikisha usalama ndio

maana alimechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuna matatizo katika uongozi na wanafunzi shuleni hapo. Alisema,

baada ya kufika Shuleni hapo, alibaini kuna tatizo la kiutawala kwa walimu na tatizo la nidhamu kwa wanafunzi, kwani

alidai wanafunzi wengi hawakuwapo Shuleni huku uongozi wa shule haujui wanafunzi hao wapo wapi. An nuur, ilipotaka

kujua uhalali wa barua ambazo walipewa wanafunzi tisa wa Kiislamu wa Shule hiyo na Bodi ya Shule kwa lengo

kuwasimamisha Shule kisha wanafunzi hao kugoma kuzipokea na kusaini, alisema hilo ni miongoni mwa mambo ambayo

Wizara itashughulika nalo katika uchunguzi wake na wanaotakiwa kuzitolea ufafanuzi ni Wizara husika.



“ M i m i s i o Wi z a r a y a Elimu, zile barua zitafanyiwa kazi na Wizara ya Elimu, wao ndio wataeleza hiyo adhabu

iliyotolewa na Bodi ni sahihi au la baada ya kujua chimbuko la mgogoro huo.” Alisema. Kufuatia kufungwa kwa Shule

hiyo, tokea jumanne wiki hii, wanafunzi wamekuwa wakiondoka kwa utaratibu maalum kurejea makwao mpaka hapo

watakapotakiwa kurejea tena shuleni hapo. Kufuatia mgogoro huo wa muda mrefu Shuleni hapo baina ya Wanafuzi wa

Kiislamu na Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Bonus Ndimbo, hali ilikuwa mbaya zaidi Jumatatu wiki hii, pale ambapo Bodi ya

Shule, ilipoamua kuwapa barua za kuwataka wanafunzi tisa wa Kiislamu kuondoka Shuleni hapo.

Baadhi ya wanafunzi wameeleza kuwa, barua hizo zilikuwa ni za kuwasimamisha wanafunzi hao ambao miongoni mwao

ni viongozi wa Waislamu Shuleni hapo, mpaka Novemba 26, mwaka huu, huku wakidai barua hizo hazikueleza sababu

za msingi wao kusimamishwa. Taarifa zaidi zinasema, wanafunzi hao walipokuwa wakikabidhiwa barua hizo kisha

kutakiwa kusaini, waligoma wakidai bado walikuwa wakisubiri majibu yao ya msingi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya

(Bagamoyo), Bw. Ahmed Kipozi, aliyefika Shuleni hapo siku chachache nyuma na kupokea malalamiko yao na kuahidi

kuwapa majibu ya kero zao dhidi ya Mkuu wa Shule hiyo. Wanafunzi wa Kiislamu Shuleni hapo, baada ya kubaini kuwa

wenzao walikuwa wanatakiwa kusimamishwa Shule, walikusanyana na kufika pale walipo wenzao mbele ya Bodi,

wakitaka barua hizo za kusimamishwa wapewe wote huku wakidai tatizo ni la wanafunzi wote wa Kiislamu. Baada ya

muda, viongozi wa Mkoa na Wilaya, chini ya Mkuu wa Mkoa, Hajjat. Mwantum Mahiza, walifika Shuleni hapo, kisha

kufanya kikao maalum baina ya uongozi na wanafuzi wa Shule, ambayo katika jumla ya mambo aliyoongea Hajjat.

Mahiza, ni kusisitiza umoja na kuvumiliana. Hajjat Mahiza, alinukuliwa akisema, kama mtu anaswali swala tano na


mwingine hawali swala hizo, ni vyema wakavumiliana kwani kila mmoja ndivyo imani yake inaruhusu hivyo. Baada ya

nasaha zake, Mkuu huyo wa Mkoa aliamuru Shule hiyo ifungwe, ili kupisha uchunguzi ufanyike kubaini kiini cha mgogoro

huo kisha hatua stahiki zichukuliwe. Awali, wakielezea chimbuko na chanzo cha mgogoro huo, baadhi ya wanafunzi wa

Shule hiyo (majina tunayahifadhi) kabla na baada ya tukio la kufungwa kwa Shule hiyo, walisema tatizo ni Mkuu wa

Shule, Bw. Bonus Ndimbo, kudhihirisha udini na chuki kutokana na kauli zake kwa wanafunzi wa Kiislamu shuleni hapo.


Walisema, Mwalimu huyo tokea ahamie shuleni hapo amekuwa akitoa kauli za kupandikiza chuki miongoni mwa

wanafunzi wa Kiislamu kwa wenzao wa Wakristo, kwa kuwaita Al-kaida, Alshabab, huku mara kwa mara

akiwatahadharisha Wakristo kuwa mbali na Waislamu. Wanafunzia hao walieleza kuwa mwanafunzi yoyote wa Kiislamu

anayeonekana kuwa anafuata maadili ya dini yake, mwalimu huyo hujenga chuki naye na kumuita Alshabab, huku

akidai kuwa atahakikisha anawapunguza Shuleni hapo. Wanafunzi hao wanamtaja mwanafunzi El-Hakim Somji, aliye na

asili ya Kihindi, kuwa miongoni mwa wanafunzi wanaoandamwa sana na Mkuu wa Shule, akimkejeli kuwa ni Al Shabab.

“Sikupendi na sitokupenda.” Wanafunzi hao walimnukuu Mkuu wao, wakidai ni maneno aliyomwambia mwenzao Somji,

huku akimshutumu kuwa ana uhusiano na Alkaida. Walisema, katika kujitete mwanafunzi Somji, ambaye pia ni Katibu

wa wanafunzi wa Shule hiyo na mweka hazina kwa upande wa wanafunzi wa Kiislamu, aliwahi kumueleza Mkuu wake


wa Shule kuwa, anaona hamtendei haki kumuita gaidi wa Al Qaida. Wanafunzi hao walibanisha kwamba, hali

ilijiridhirisha zaidi, kipindi cha uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi kilipofika ambapo Mkuu huyo, alibadili mfumo uliokuwa

ukitumiwa miaka yote shuleni hapo, kwa kila nafasi inayogombewa ilikuwa na watu watatu, lakini kwa utaratibu mpya

kila nafasi alitaka iwe na wagombea wawili, tena Mkristo na Muislamu. Walisema, siku moja kabla ya uchaguzi, Oktoba

3, mwaka huu kupitia katika sanduku la maoni Mkuu wa Shule aliwataja wanafunzi Ramadhani Bilali, na Kaiza

Ruttakinikwa kidato cha Sita CBG, kuwa wanafunzi hao wanashawishi udini Shuleni hapo. Siku ya uchaguzi, (Oktaba

42012), majira ya asubuhi, Mkuu huyo inadaiwa alikwenda na karatazi hiyo ya maoni katika darsa la wanafunzi hao

kisha kuisoma na kabla ya kuisoma alimtaka Ramadhani Bilali, akamsubiri ofisini kwake. Inadaiwa kuwa, akiwa darasani,

Mkuu huyo anadaiwa kusema kuwa kuna watu wanajifanya kujua sana dini Shuleni hapo, huku akiwashawishi


wanafunzi kutowasikiliza na kuwapuuza kama watu wa sokoni. “Kuna watu hawapaswi kufuatwa, mfano kama hawa

wanaoswali swali sana, kutwa nzima wanaswali tu. Mwenyezi Mungu ameweka siku moja tu ya kuswali.” Kilisema

chanzo chetu, kikimnukuu Mkuu huyo. Imeelezwa kuwa akitoa lawama hizo darasani, mwanafunzi aliyetajwa kwa jina la

Japhet Kazimili (Mkristo) alipingana na Mkuu huyo, akisema kuwa huenda taarifa hizo amezipata tofauti kwani alidai,

hakuna udini kama anavyodai (Mkuu). Chanzo chetu kilisema, Mkuu huyo alimtuhumu mwanafunzi Ramadhani Bilali

ambaye ni kiongozi wa wanafunzi wa Kiislamu kuwa ni Alshabab na ni mdini na kuwa hayupo peke yake Shuleni hapo.

Siku hiyo ya Oktaba, 4, 2012, ambayo ndiyo ilikuwa siku ya uchaguzi wa wanafunzi, wakiwa mstarini Mkuu wa Shule,

aliisoma ile barua ya maoni kisha alitoa orodha ya wanafunzi Ramadhani Bilali (Kiongozi wa Da’awa na taaluma kwa

Waislamu), Kaiza Ruttakinikwa, El-Hakim Somji, Answaar Abdulhakim, Amin Thabit (Amir wa Jumuiya ya wanafunzi wa

Kiislamu), akisema anawatahadharisha na watu hao sana Shuleni hapo, kisha aliakhirisha uchaguzi huo na kusema

utafanyika siku inayofuata, Oktoba 5, 2012. Kufuatia kauli hizo za Mkuu wa Shule, wanafunzi Waislamu waliokuwa

wakigombea katika nafasi mbalimbali waliandika barua za kujitoa katika uchaguzi, kwani miongoni mwa waliotajwa siku

hiyo miongoni mwao ni wagombea, hivyo walidai Mkuu alidhamilia kuvuruga uchaguzi kwa kuwatangazia sifa mbaya

mbele ya wapiga kura (wanafunzi). Hata hivyo uchaguzi huo uliendelea siku hiyo huku wanafuzni wa Kikristo

wakinukuliwa wakitamba kuwa wanaenda ‘kusimika Kanisa’, huku Mkuu akisema, kujitoa kwa wagombea hao wametumia

demokrasia yao hivyo hawezi kuahirisha uchaguzi hukuakionyesha kuridhishwa na hali hiyo. “ Tu l i a n d i k a b a r u a

k w a Mkuu kuonyesha kuchoshwa na mwenendo wake mzima na kwamba anapandikiza mbegu za udini na

kutengeneza matabaka miongoni mwa wanafunzi shuleni hapo ambao kabla ya ujio wake matatizo hayo hayakuwepo.”

Alisema mwanafunzi mmoja. Oktoba 15, mwaka huu, waliamua kuelekea kwa Mkuu wa Wilaya kupeleka malalamiko yao,

hata hivyo njiani walikutana na Jeshi la Polisi, na kuwazuia na walipoulizwa walieleza nia yao ya kumuona Mkuu. “Polisi

walituomba turudi na kutuitia Afisa Elimu wa Wilaya (D.E.O), Mwl. Majoyo, ambaye tuliamini ni mtu ambaye atatusaidia

kutatua matatizo yetu na Mkuu wa Shule, baada ya kutusikiliza alihaidi kulifanyia kazi na kututaka kurudi madarasani ili

amsikilize na Mkuu pia kabla ya kutoa majibu ya pamoja.” Alisema


Source: Annuur
 
An nuur, ilipotaka

kujua uhalali wa barua ambazo walipewa wanafunzi tisa wa Kiislamu wa Shule hiyo na Bodi ya Shule kwa lengo

kuwasimamisha Shule kisha wanafunzi hao kugoma kuzipokea na kusaini,


Source: Annuur

Nilianza kuisoma vizuri ilipofika kwenye kwenye source yenyewe ya habari na kugundua ni hiyo kwenye nyekundu ikapoteza credibility yote ya habari.. Mkuu tafuta a reliable source maana inaonekana kuna tatizo lakini hawa wanaripoti from their angle..
 
Hili gazeti la Annur sidhani kama linawasaidia waislamu, pale linapoandika uwongo na kueneza chuki ya udini.

Mimi Mwenywe kwa macho na masikio yangu nilimuona na kumsikia ITV Hajjat Mahiza akisema kwamba hao wanafunzi tisa wa Kiislamu walisimamishwa shule kwa makosa, kwanza WALIMBAKA MWALIMU wao, read again walimbaka! Pili walikwenda kuogolea baharini na kufanya FUJO kwa KUWAPIGA watu.

Akahitimisha kwamba mgogoro ulipo Bagamoyo Sekondari sio wa KIDINI. Bali watu wachache wanataka kuufanya uonekane wa KIDINI. Sasa nimejua kumbe alikuwa analilenga pia gazeti hili Annur.

Bila aibu eti leo Annur linawatetea hao wanafunzi MAFIRAUNI tena kwa kuandika UONGO. Kwa mwendo huu wa Annur I don't see any light at the end of the tunnel for my muslims brothers and sisters.
 
Mhariri angewashauri wagomee mitihani kama wale wa lindi. Shuleni watu wanaenda kueneza dini eeh? Mmenikumbusha rafiki yangu wa chuo, tukiwa na test anakesha akisali na kuomba anajigalagaza sakafuni. Akitoka kusali yuko kama0 chizi. First year alidisco kichwa chini miguu juu. Mungu hamtupi mja wake, ni kuli airport ya kilimanjaro (swissport)
 
Juzijuzi tu Nchimbi alipotoa tamko kuwa waliochoma Makanisa ni wahuni alikomaliwa hapa na tukapewa taswira ya kuwa wanasiasi ni watu ambao kauli zao haziaminiki!
Ni kitu gani leo kimekufanya mwenzetu uishadidie na kuiamini kauli ya mwanasiasi mwengine kam sio chuki
zinazokusumbua?!..tujuze.
 
Hivi kwa nini hawa Watu wasiwahase Vijana wao Mara waendapo shule Wazingatie Elimu!! Au wakiambiwa wazingatie elimu wao wanaona Ni kuonewa?
 
Hakika kafiri ni adui wa mwislamu
 
Waislamu wangetoa mentality ya kwamba wao wanaonewa na kufanya juhudi katika shughuli za maendeleo na kumtafuta Mungu wao wangekuwa wanafanya kitu cha maana zaidi ya kupteza muda wa kumtafuta mchawi.
 
Mwanahalisi limefungiwa kwa kuandika ukweli, lakini magazeti yanayochochea udini yanaachwa, na ni kwa maelekezo ya kikwete na ndio maana yupo kimya na kama anazungumzia huwa anagusia tu, akijifanya anakemea kumbe ndio mfadhili na mdhamini mkuu.
 
Hayo matoto mavilaza na yanauhakika wa kufeli ndo maana yanaleta fujo the samewise hata wanaochoma makanisa ni wale choka mbayaaaa waso na hali. Hizi dini zenyewe tumeiga kwa wakoloni (waingereza) na wafanyabiashara ya utumwa (waarabu) leo tunajifanya tuna uchungu kuliko wao kama kweli uchungu umewashika waende leba shaabashhh.
NB: sikio halizidi kichwa
 
Badala ya kubishana source ipi ya habari iko sahih,acha tusubiri ripot ya uchunguz ndo tutaujua ukweli.
Vyombo vya habari vya bongo vinatatizo la kupotosha uhalisia wa habari.
 

wewe ndo hujafuatilia hyo habar au aliekuwa anatoa ndo amepotosha.wanafunz wanalio tuhumiwa kumbaka mwalim ni form 6 walio maliza mwaka 2012 hao walikuwa form5 sasa wanauhusiano gan na hyo case au ndo kuwatengenezea mazingira kuonekana wabaya!?
 
N aibu kubwa sana kuona mtanzania mwenye akili timamu anashare thread ya kipumbavu isiyokua na uhalisia wowote kama hii, GUYS I DONT CARE OF ANY RELIGION BT I KNOW WELL MR NDIMBO, binadamu shukran hatuna, pamoja na yote aliyoyafanya pale bagamoyo hivi ndivyo tnavyomlipa? If you care alot for religion hamien saud arabia tuachien nchi yetu.
 


Hii nchi ni ya kwetu sote, panapo ukweli na usemwe............kumjua mtu vizuri haina maana hafanyi makosa, huwezi kusemwa vibaya na kila mtu
 
Wewe hujaelewa na nadhani hutaki kuelewa, kuswali swala 5 haina maana unaeneza dini bali ni utaratibu wa lazima kwa waislamu. Kwahiyo inapotokea mtu anakuzuia manake hakutendei haki kabisa. Kama huyo Mwalimu Ndimbo kafanya kuwakejeli kweli basi ni mpuuzi na hajitambui anaishi dunia ipi bali analipua bomu na waislam. Ni hayo tu
 
Hata afanye mazuri gani lakini akiwa mdini atoke zake. Yani aachiwe azidi kueneza propaganda zake walizoshindwa mabwana zenu wa magharibi eti Gaidi Muislamu non sense na shame on him! Fukuza huyo mwalimu asije kuzidisha hali tete huko. Hii CD/movie ya Ugaidi ishafeli tafuteni nyingine. Wafu
 
Badala ya kubishana source ipi ya habari iko sahih,acha tusubiri ripot ya uchunguz ndo tutaujua ukweli.
Vyombo vya habari vya bongo vinatatizo la kupotosha uhalisia wa habari.
Dunia nzima kila chombo cha habari kinamsikiliza bwana wake anataka nini. We unatarajia TV za bongo wataonyesha au kuchambua kitu sahihi! Uzuri watu washaelimika huwa wanawapuuza tu iwe habar ya kisiasa, uchumi etc. Habar ya kuiamini kwenye TV za bongo ni msiba tu wakitangaza tena waonyeshe na picha. Umenielewa nadhani..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…