mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Hili gazeti la Annur sidhani kama linawasaidia waislamu, pale linapoandika uwongo na kueneza chuki ya udini.
Mimi Mwenywe kwa macho na masikio yangu nilimuona na kumsikia ITV Hajjat Mahiza akisema kwamba hao wanafunzi tisa wa Kiislamu walisimamishwa shule kwa makosa, kwanza WALIMBAKA MWALIMU wao, read again walimbaka! Pili walikwenda kuogolea baharini na kufanya FUJO kwa KUWAPIGA watu.
Akahitimisha kwamba mgogoro ulipo Bagamoyo Sekondari sio wa KIDINI. Bali watu wachache wanataka kuufanya uonekane wa KIDINI. Sasa nimejua kumbe alikuwa analilenga pia gazeti hili Annur.
Bila aibu eti leo Annur linawatetea hao wanafunzi MAFIRAUNI tena kwa kuandika UONGO. Kwa mwendo huu wa Annur I don't see any light at the end of the tunnel for my muslims brothers and sisters.
Hapo kwenye red inaniumiza sana
Kila siku nasema waislam tukemee na tukatae kutumika kwa maslahi ya watu...
kama leo tukilinyamazia hili la mwalimu kubakwa kesho watatubaka hata sisi wazazi wao
Tupendane jamani eh