tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imemzawadia Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Nsumba, Denis Mwakisimba, gari aina ya Toyota IST kutokana na mchango wake mkubwa katika kuinua kiwango cha ufaulu wa shule hiyo, ambayo imeendelea kufanya vizuri kwa mfululizo.
Soma pia: Wakuu wa shule wabadilishwe vituo vyao vya kazi kila baada muda fulani
Tukio hilo limefanyika jana, Agosti 6, 2025, ambapo pia walimu wa shule hiyo wameahidiwa kugawiwa zaidi ya shilingi milioni 18 kama motisha ya kuendeleza juhudi zao za kufundisha na kuinua viwango vya elimu.
Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, aliwataka walimu wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii bila kujali nafasi au cheo walicho nacho, akieleza kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuweka alama ya mafanikio.
“Nimeambiwa kuwa Mkuu huyu wa shule popote alipokwenda ameacha alama. Haiwezekani mtu ukae sehemu miaka mingi bila mchango wowote unaoonekana. Tafuteni sehemu mnapoweza kung'ara, wekeni alama zenu,” alisema Mtanda.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, alibainisha kuwa pamoja na juhudi za Mkoa kutoa motisha kwa shule, walimu na wanafunzi, Halmashauri inaendelea na mpango wa kuwatambua na kuwazawadia wale wanaosaidia kuinua ufaulu, hasa katika elimu ya msingi.
Kwa upande wake, Mwalimu Denis Mwakisimba alishukuru kwa kutambuliwa, na kuahidi kuendelea kushirikiana na walimu pamoja na uongozi wa serikali kuhakikisha kiwango cha elimu mkoani kinaendelea kupanda.
Tukio hilo limeambatana na utoaji wa tuzo na zawadi mbalimbali zilizoratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwa ajili ya shule, walimu na wanafunzi waliotoa mchango mkubwa katika kuinua ufaulu mkoani humo.
Chanzo:Nipashe