Mkuu wa shule Igoma sekondari ya Mwanza anaongoza shule kwa makundi

masanzaone

Member
Joined
Jul 7, 2013
Posts
6
Reaction score
1
Mkuu wa shule ya sekondari Igoma iliyoko jijini Mwanza bwana Bregrey j. Nyakyuma amesemekana kuongoza shule kwa kuwagawanya makundi walimu wake huku akionesha udhaifu mkubwa kwa upande wa walimu wa jinsia ya kike.

Taarifa kutoka shuleni hapo zinaonesha walimu wameonekana kukerwa na tabia na mwenendo mzima wa uongozi wa mkuu huyo wa shule ya sekondari Igoma huku wengine wakilalamikia kuwa uelewa mdogo wa baadhi ya wakuu wa shule katika masuala mazima ya uongozi ni changamoto kubwa katika uendeshaji wa shule hizi za sekondari ikiwa ni pamoja na mkuu huyu wa sekondari Igoma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkuu huyu imesemekana pia kuwa na mawazo mgando yaani mkuu asiyeweza kuenenda na hali ya mabadiliko au kushaurika.

Mkuu huyu ameonesha udhaifu mkubwa na kusemekana kuwa mwalimu yeyote anaeonekana kupingana nae kimawazo uchukua jukumu la kupigana nae maamuzi ambayo ni ya kijima katika ulimwengu huu wa sayansi na tecknolojia na kwa kiongozi yeyote.

Baadhi ya walimu wamekuwa wakiondoka katika shule hiyo. Hata hivyo tuna wasiwasi mkubwa juu ya uteuzi wa mkuu huyu kama ulifuata vigezo maana uwezo wa kuongoza shule ni mdogo kwa mkuu huyu wa shule mambo ambayo yanapelekea kushusha kiwango cha utendaji kazi mashuleni.
 
  • Thanks
Reactions: Pus
Sio mawaziri tu hata wakuu wa shule mizigo wapo.Mzigo mzto kabsa uko Meatu sec. huyu anabebwa na DEO Nkonde.bonge y mzgo
 
Umeandika mengi lakini hakutoa hata mfano mmoja ili kutetea hoja yako. Kwangu mimi huu ni umbea uliopitiliza na ningekua na uwezo ningewaomba mods wafute huu uzi, umbea mtupu.

Tiba
 
pole mwalimu ila kumbuka wewe ni miongoni mwa wanaotengeneza makundi shuleni, kisha unakimbilia huku kwenye jukwaa.Acha majungu jadilini matatizo yenu kwenye vikao husika ,huku mkuu wako inawezekana hata si member .Kumbuka vikao vya mara kwa mara vinaondoa majungu .
Mkuu wa shule ya sekondari Igoma iliyoko jijini Mwanza bwana Bregrey j. Nyakyuma amesemekana kuongoza shule kwa kuwagawanya makundi walimu wake huku akionesha udhaifu mkubwa kwa upande wa walimu wa jinsia ya kike.

Taarifa kutoka shuleni hapo zinaonesha walimu wameonekana kukerwa na tabia na mwenendo mzima wa uongozi wa mkuu huyo wa shule ya sekondari Igoma huku wengine wakilalamikia kuwa uelewa mdogo wa baadhi ya wakuu wa shule katika masuala mazima ya uongozi ni changamoto kubwa katika uendeshaji wa shule hizi za sekondari ikiwa ni pamoja na mkuu huyu wa sekondari Igoma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkuu huyu imesemekana pia kuwa na mawazo mgando yaani mkuu asiyeweza kuenenda na hali ya mabadiliko au kushaurika.

Mkuu huyu ameonesha udhaifu mkubwa na kusemekana kuwa mwalimu yeyote anaeonekana kupingana nae kimawazo uchukua jukumu la kupigana nae maamuzi ambayo ni ya kijima katika ulimwengu huu wa sayansi na tecknolojia na kwa kiongozi yeyote.

Baadhi ya walimu wamekuwa wakiondoka katika shule hiyo. Hata hivyo tuna wasiwasi mkubwa juu ya uteuzi wa mkuu huyu kama ulifuata vigezo maana uwezo wa kuongoza shule ni mdogo kwa mkuu huyu wa shule mambo ambayo yanapelekea kushusha kiwango cha utendaji kazi mashuleni.
 
Siwezi shangaa kuhusu hili hata kidogo. Hili ni tatizo kubwa sana hasa kwetu sisi walimu. Wakuu waliowengi hasa shule binafsi hugawa nguvu kazi ndipo waweze kuwaongoza. Kwa hiyo vikao mara nyingi naona ni kelele na kupoteza mda kwani na wala havina msaada wa moja kwa moja katika kutatua matatizo kama haya. La kufanya ni kufanya kazi na kutimiza majukumu yako kama mwalimu na inapozidi fanya upate uhamisho.
 
Back
Top Bottom