Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 879
- 814
Habari za muda huu ndugu wapenzi wa jukwaa hili la JamiiForums.
Kuna Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Ikulu iliyopo jijini Mbeya, anaye julikana kwa jina la Godfrey Sitayila amekuwa kero kubwa sana kwa wazazi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo.
Amekuwa akitoa kauli ambazo siyo nzuri kwa wazazi. Mtoto anaweza kufanya kosa na kuamuliwa kumleta mzazi na pindi mzazi anapotii na kufika shuleni hapo, mkuu huyo badala ya kumsikiliza mzazi anaendelea na mambo yake hata zaidi ya masaa mawili kitu ambacho kimekuwa kero kwa wazazi wengi.
Pia mkuu huyo amekuwa anatoa adhabu kali kwa wanafunzi hali inayopelekea wanafunzi kuichukia shule.
Wazazi wanapoenda kuwaombea watoto ruhusa anawatishia kuwafukuza shule au kuwahamisha watoto hao.
Ombi la wazazi kwa serikali ni kutaka kumkanya mkuu huyo wa shule ya sekondari Ikulu kuacha kiburi kwa wazazi.