Mkuu wa usalama Marekani ajiudhuru

Mkuu wa usalama Marekani ajiudhuru

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
13,265
Reaction score
4,735
Mkuu wa Usalama Marekani ajiuzulu.

Mkuu wa Idara ya Usalama nchini Marekani, aliyekuwa na jukumu la kumlinda Rais Barack Obama, amejiuzulu kufuatia matukio yenye kuhatarisha usalama wa taifa yaliyotokea.

Mkuu huyo wa usalama Julia Pierson alikabidhi barua ya kujiuzulu kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Jumatano.

Siku moja kabla, alikabiliana na maswali ya wajumbe wenye hasira kutoka Baraza la Congress juu ya udhaifu mkubwa wa usalama wa Ikulu ya Marekani

Habari za tukio lingine likimhusisha mtu mwenye silaha kuruhusiwa kuingia katika lifti moja na Bwana Obama kulizidisha kutolewa wito wa kumtaka mkuu wa usalama kujiuzulu.

"Leo, Julia Pierson, mkurugenzi wa usalama wa taifa wa Marekani, amenikabidhi barua ya kujiuzulu, na nimeikubali," Waziri wa Usalama wa Taifa Jeh Johnson aliandika katika taarifa.

"Nampongeza kwa utumishi wake wa miaka 30 katika idara ya usalama na taifa."

News
Nyumbani
ENG | KIS © Tigo
 
Nimesoma kwamba kuna mtu alipanda lift.moja na Obama huku ana silaha...hatari sana nadhani alipaswa kujiuzulu
 
Wenzetu wanajuwa kuwajibika;
Kwetu ni siasa za bla bla tu;
 
na ukizingatia Rais ni mweusi, hiyo haikuwa bahati mbaya
 
Itatuchukua miaka mingapi kufikia level hiyo ya weledi?
 
Kapigwa maswali na Congress kashindwa kujieleza matokeo mengi yametokea white house tangu Obama awepo madarakani
 
Sijui lini akina mbowe watajifunza uwajibikaji ndani ya vyama vyao? Kuzaa nje ya ndoa ni kashfa kubwa sana kwa kiongozi wa taasisi alitakiwa kujiuzulu.

Kula milion 100 hela za fisadi Rostam ni kashfa kubwa ndani ya taasisi alitakiwa kujizulu.

Kula milion 100 hela za fisadi Nimrodi mkono ili mwenyekiti asipeleke mgombea ubunge jimboni kwa mkono ni kashfa kubwa sana kwa kiongozi wa taasisi alitakiwa kujiuzulu.

Kula hela za chama zilizotolewa kama msaada na kwenda kuanzishia gazeti binafi ni kashfa kubwa sana kwa kiongozi wa taasisi alitakiwa kujiuzulu.

Mwenyekiti Kukiuzia chama mafuso chakavu kwa bei ya kiwandani ni kashfa kubwa sana alitakiwa kujiuzulu.

Katibu wa chama mwenye miaka 67 kuishi maisha ya uchumba ni kashfa kubwa sana alitakiwa kujiuzulu.

Waafrika kuwajibika sio utamaduni wetu.
 
Sasa hapa Mbowe anaingiaje?
 
Uungwana ni kujitambua na kujua maana ya dhamana uliyopewa! Hapa kwetu tumefanya Utumishi wa umma kuwa ajira isiyo na mipaka! Its soooo distressing!
 
Back
Top Bottom