#COVID19 Mkuu wa WHO atoa wito kwa G20 kumaliza mzozo wa chanjo

#COVID19 Mkuu wa WHO atoa wito kwa G20 kumaliza mzozo wa chanjo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa Kundi la mataifa 20 yaliostawi na yanayoinukia kiuchumi G20 yana uwezo wa kuzuia janga la virusi vya corona kuenea zaidi na kuzuia majanga ya siku zijazo.

Akizungumza wakati wa mazungumzo kuhusu afya hapo jana kwenye mkutano wa G20 mjini Roma, Ghebreyesus alitoa wito kwa wanasiasa kumaliza mzozo kuhusu chanjo kwa kushughulikia uhaba wa dozi za chanjo hizo kwa mataifa maskini.

Ghebreyesus ameongeza kwamba wanaelewa na kuunga mkono wajibu wa kila serikali wa kulinda raia wake lakini akasema kuwa usawa wa chanjo sio hisani ila ni la manufaa ya kila nchi.

Alitoa wito kwa mataifa hayo ya G20 kusambaza kwa haraka misaada ya chanjo iliyokuwa imeahidiwa na kuunga mkono utengenezaji wa chanjo barani hizo Afrika.

Chanzo: DW Swahili
 
Back
Top Bottom