Kuna tatizo nimeligundua hapa,watu wamecomment pasi na kujua mantiki ya mleta mada ni ipi . Hii naifananisha na pale unapomuuliza mtu eti Tanzania ilipata uhuru mwaka gani,nae bila kujua mantiki ya swali akajibu 1961. Wakati kumbe Tanzania imekuwa Tanzania mwaka 1964 baada ya nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar kujiunga. Sasa nikirudi kwenye mada lazima tujue mleta hoja alilenga nini. Hoja hapa sio ya kichama,ni ya kitaifa,kila chama kina muongozo wake na hakina direct effect kwa taifa. Chama kina miongozo katika kupata viongozi na mara nyingi hutumia kura km njia ya kujipatia viongozi wao. Hvy kuwa na ndugu wa moja kwenye uongozi wa chama kimoja sio kosa la chama,kura imeamua,na hakuna direct cost kwa taifa. Ukija kiserikali,kuna nafasi za kugombea na kuteuliwa. Unapogombea ukachaguliwa na ukavurunda waliokuchagua itawa cost,ila unapoteuliwa na kuvurunda wakulaumiwa ni aliyekuteua. Mantiki ya mleta hoja ni je,ikiwa aliyeteuliwa ni mtoto wa kufikia wa aliyemteua,,ikifikia wakati wa kuwajibishana atamuwajibisha? Kuwa mtoto wa kufikia si sababu ya kupimia upendo wa kifamilia. Zipo familia nyingi wanathamini zaidi watoto wa kufikia kuliko wa kuwazaa . Sàsa je kama huyu nae ni kipenzi cha aliyemteua,atakapovurunda atawajibishwa? Hapa tunaangalia mustakabali wa nchi sio chama. Tusijenge hoja kwa mizuka ya kichama,tuwe wazalendo linapokuja suala la kitaifa. Vyama vipo na mtu unaweza kuhama muda wowote ila sio uraia/utaifa.Nimemaliza