abdullahsida
Member
- Nov 21, 2015
- 26
- 2
Hata kama angekuwa baba yake ulitaka huyo binti afanye kazi gani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio "hata angekuwa baba yake"....Happy ni mwanae wa kumlea, alisoma Ualimu chuo cha Ualimu Kigurunyembe pale Morogoro,baada ya Diploma yake akajiunga na Chuo Kikuu Dodoma kwa njia ya "Equivalent/Mature Entry".Dodoma alijiunga kwa Degree ya Education,lkn wakati huo "Mzee" akiwa Ujenzi akambadilishia Degree na kumpeleka BBA(Kumbuka wapo wengi waliotaka kubadili toka Education kuja BBA)Hata kama angekuwa baba yake ulitaka huyo binti afanye kazi gani
Ni mzuri kama yule mrefu mweusi ambatanisheni na kapicha basi
Kama ana sifa hamna shidaHapa kila MTU mahali ulipo wewe vuta ndugu yako weka ukiulizwa sema tatizo ni mfumo!
Mimi naona bado katika kuwateua wakuu wa wilaya kuna haja ya kuwateua "wataalamu wa maabara" na si wafanya majaribio! nina maana watu wanatakiwa wapewe kazi za kiutawala za kawaida ndani ya serikali ndipo wapewe ukuu wa wilaya. Ukuu wa wilaya si lazima uwe na elimu kubwa bali hazina kubwa ni uzoefu katika utawala mfano mtu akiwa katibu tawala au mkurugenzi au katibu tarafa ataweza ukuu wa wilaya vizuri. hata katibu wa chama wa wilaya anaweza kuwa mkuu wa wilaya mzuri.Happy amesoma na mdogo wangu wa kike UDOM....mimi huwa nadhani ni mwanae kabisa JPM,kumbe ni wa kumlea tu!!ana elimu nzuri japo sina hakika na uwezo wake wa kiungozi
Mdada ana bahati sana. Anapata ufadhili wa kufanya Masters na kampuni moja ya Ujenzi wa miundombinu toka China! Hivi huo ufadhili haukuwa na masharti? Ama kweli nchi hii imetafunwa sana, kampuni inaamua kumfadhili mtoto wa mkubwa kwa masharti yasiyoeleweka!?.Sio "hata angekuwa baba yake"....Happy ni mwanae,huyu alisoma Ualimu chuo cha Ualimu Kigurunyembe pale Morogoro,baada ya Diploma yake akajiunga na Chuo Kikuu Dodoma kwa njia ya "Equivalent/Mature Entry".Dodoma alijiunga kwa Degree ya Education,lkn wakati huo "Mzee" akiwa Ujenzi akambadilishia Degree na kumpeleka BBA(Kumbuka wapo wengi waliotaka kubadili toka Education kuja BBA)
Wakati huo mkuu wa School of Social Science hapa UDOM alikuwa Profesa Baradyana(Marehemu,kwa tuliosoma UDSM tunamkumbuka).Alipomaliza Dodoma akaenda kufanya Masters China kwa "msaada" wa kampuni moja ya Ujenzi wa miundombinu toka China,aliporudi tu akapewa nafasi ya Umeneja wa Rasilimali Watu huko TANROADS.Mwaka 2010 alipomaliza chuo aligombea viti maalumu kwa vijana lkn kura hazikutosha.Huyu ndio Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kisarawe.Tunamtakia Kazi Njema huko kwa Wazaramo!!
Hamjifunzi kwa mataifa makubwa ka USA,clintony alikuwa Rais na sasa mkewe anagombea hapa a shaka atapata sasa ingekuwa bingo hii pasingetosha kama anavigezo kwanini asipewe nafasi??tuache
majungu.
Tatizo liko wapi? kwani umekatazwa kwenda shuleMara baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya uliofanyika na kutangzwa leo, jamii imeanza kuwachambua na kujuwa historia zao na ushiriki wao katika kumasaidia kazi Mh Rais.
Wananchi wamekuwa na shauku ya kumfahamu na kuelewa historia ya Mkuu wao mpya wa Wilaya Mh. Happynes Senenda William. Kabla ya kuwa DC wa Kisarawe tunaambiwa dada huyu alikuwa Manager wa HR wa TANROADS Mkoa wa Tanga, ni mdada mdogo mwenye elimu ya Masters. Mwaka 2010 aligombea ubunge viti maalumu kupitia mkoa wa Geita lakini hakufanikiwa, mwaka 2015 alipumzika ili kuzunguka na baba kumtafutia kura
Habari zinazidi kupenyeza kuwa Mh.Happyness William ni mtoto wa kulelewa na Rais JPM, amesomeshwa na Rais na amekuwa akiishi na JPM kwa maisha yake mpaka alipopata kazi. Kifupi Mh.Happyness ni "mtoto" wa JPM na kwa sasa ni DC wa Kisarawe
Ama hakika huu ni msimu wa vijana...Vijana mjiibidishe ili muonekane na mpate Wilaya au Mkoa.
Hakika.Nepotism rearing it's ugly head
Kazi ipo kweli kweli...!!Kazi ipo
Nepotism ni aibu kwa wahusika wote ndiyo maana tunahitaji anti nepotism laws. Trump anahaha kuajiri watoto wake lakini sheria zinamkataza.Wewe unaelewa maana ya conflict of interest au unaleta ushabiki maandazi hapa. Huyo mteuliwa kwa misingi ya undugu anaweza akatumia madaraka vibaya kwa kuwadhulumu watu au kuwanyima haki kwa vile ameteuliwa kwa misingi ya nepotism. Hata kama anazo sifa, hakutakiwa kumpa nafasi kama ya ukuu wa wilaya ambayo ina uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya "Baba" yake. Je atawatendea haki wapinzani wa "baba" yake? Je mkuu wa mkoa atakuwa na uhuru wa kumuwajibisha "mtoto wa raisi"?
Kama hii habari ni ya ukweli basi tukubaliane kuwa misingi ya utawala bora imekiukwa na ifikie wakati haya mambo yawepo kwenye katiba ya nchi.
Kama ni kweli je nepotism si inarudisha nyuma maendeleo?Tatizo reliability ya information zinazozunguka kwenye mitandao yetu ya kijamii iko chini sana. The veracity of your conclusion about anything depends on the veracity of the basis for your conclusion! Garbage in garbage out. It's that simple!
Teteeni tu lakini huyu Mheshimiwa ana tabia hii ya nepotism.Mkuu inabidi urudi darasani hujui nini maana ya conflict of interest. Mkuu wa wilaya ni mwakilishi wa rais wilayani. Unapozungumzia conflict of interest always Ina involves two parties. Sasa hiyo conflict of interest ni Kati ya Nani na nani
Hupaswi kuwateua ila nafasi za kuchaguliwa ni rukhsa.Hivi ukiwa Raisi halafu ukawa na watoto wa kuwazaa kumi, halafu watoto wamesoma kwelikweli na ni wazalendo haswa, na wachapa kazi makini, Je ukiwateua Zile nafasi Kumi za Ubunge kisha Ukawapa Uwaziri Litakuwa ni Tatizo?
Je Ukifanya hivi, Makatibu wa Kuu wa wizara wanazoziongoza wataweza kweli kuwakatalia "Watoto wa Raisi" iwapo wataanza kufanya madudu?