Mkuu wa Wilaya Temeke akabidhiwa madarasa 157 ya Shule za Sekondari

Mkuu wa Wilaya Temeke akabidhiwa madarasa 157 ya Shule za Sekondari

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
MKUU WA WILAYA TEMEKE AKABIDHIWA MADARASA 157 YA SHULE ZA SEKONDARI

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mheshimiwa Jokate Mwegelo ameshiriki katika hafla ya makabidhiano ya Madarasa mapya 157 yaliyojengwa katika Shule 24 za Sekondari iliyofanyika leo Januari 03, 2022 katika Shule mpya ya Sekondari Dovya iliyopo Kata ya Chamazi wilayani humo.

Katika hafla hiyo Mhe. Jokate amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha fedha Bilioni 3.14 za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa, na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa hayo ulioanza Novemba 1, 2021 na kukamilika Disemba 31, 2021 vitakavyoondoa changamoto ya madarasa kwa muhula wa masomo wa mwaka 2022.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika miradi inayotekelezwa na serikali, ili kuwafanya kutambua matumizi ya mapato yanayokusanywa na halmashauri yao kwa maendeleo ya Temeke, huku akitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi na walezi kuwahimiza watoto wao wafike shule kwa wakati, kwa sababu madarasa hayo yamejengwa kuimarisha elimu ya sekondari nchini.

“Miradi yote ya maendeleo lazima tushirikishe Wananchi ili wajionee 'laivu' bila chenga, tutaendelea kuwashirikisha Wananchi kuanzia miradi inapoanzishwa, inapoendelea, inapokamilika, mapato, matumizi na hata kwenye uzinduzi kuwaomba wawepo ili kuona kwa vitendo na sio kusimulia tu” alisema Mhe. Jokate

Aidha Mhe. Jokate ametoa wito kwa viongozi wa bodi za shule za Sekondari kuendelea kukaa vikao kazi muhimu, ili kuendelea kujadili namna bora ya usimamizi wa shule, kuinua maendeleo ya elimu, na kukuza viwango vya ufaulu wa wanafunzi ili kuipaisha Wilaya ya Temeke katika ramani bora ya elimu nchini.

Aidha Mkuu huyo alishukuru kwa umoja, ushirikiano na uwajibikaji wa Mstahiki Meya, Naibu Meya, Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa, Madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Kaimu katibu mkuu wa CCM, Walimu, Watumishi wa halmshauri, pamoja na Wananchi ambao walihudhuria hafla hiyo k

IMG-20220103-WA0288.jpg


IMG-20220103-WA0282.jpg


IMG-20220103-WA0271.jpg


IMG-20220103-WA0278.jpg
 
Mama anaupiga mwingi. Mitano tena kwa mama.

Mama Pokea salamu toka kwa Spika: NIMEKOSA MIMI NIMEKOSA MIMI NIMEKOSA SANA....
Hili ungamo natamani Samia angelisikia sema ndo vile akija kukaa sawa atasimuliwa......
 
Hili ungamo natamani Samia angelisikia sema ndo vile akija kukaa sawa atasimuliwa......
Ungamo huwa tunalisali tukiwa tumepiga magoti wakati misa ikiwa ndio kwanza imeanza padre kabla hajaenda mbali anatuamuru tutubu madhambi yetu.
 
Back
Top Bottom