Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Zanzibar, Rashid Simai Msaraka amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Sekondari ya Forodhani kwa lengo la kufanya msako wa Wanafunzi wanaotumia shisha zinazotumia umeme pamoja na simu.
DC huyo amefika Shuleni na kuamuru Wanafunzi wote washushwe parade na kusachiwa mmojammoja ambapo mabegi yao yaliyoachwa madarasani nayo yalisachiwa ndipo alipokutana na shisha ya umeme moja na simu.
Amesema huenda ziara yake ya kushtukiza ilishtukiwa kabla kwani katika baadhi ya Shule alizopita alifanikiwa kukamata simu na shisha zaidi ya moja.
DC Simai ametoa onyo kwa Wanafunzi kutokwenda Shuleni na shisha, simu, spika za bluetooth, manukato na kucha za rangi pamoja na vikuku.
Pia soma:
Zanzibar kupiga marufuku shisha na sigara za kielektroniki
Marufuku nyingine Zanzibar soma:
Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika