Kuna mwandishi mmoja ameandika kitabu chake akakipa kichwa cha habari "Rulers of the law against rule of the law" u
kimsingi mwandishi anaongelea watu wa sampuli hii ya mheshmiwa wa wilaya ambao kwa utashi wanafikiri juu ya sheria na siyo kwa kufuata sheria, binafsi pia sipendezwi na mavazi ya vi-sister duu na vi- brotherman na wale wa kata k lakini nadhani ili kuwe na mizania sahihi ni vyema sheria itamke kipimo cha kutofautisha mavazi ya kimaadili na yale yasiyo ya kimaadili, lakini kubwa zaidi ni kupata watu safi watakao weza kusimamia sheria hiyo isiwe kama wanvyofanya polisi wao wanaendesha magari mabovuu kabisa tena yanatoa moshi balaaa lakini wakiona gari ya mwananchi wa kawaida wanaikamata na kutoa makosa kibao. maana yake ni kua makatazo ya mavazi hasi hayawezi kufanikiwa kama hakuna mfano wa mavazi sahihi na watu kama hawajui faida na hasara ya kuvaa nusu uchi wanakua kama wenda wazimu. angalia mfano uko kwenye daladala umebahatika kupata siti wengine wamekosa hivyo wamesimama mko kwenye foleni jua la dar linawaka kama kawaida yake joto kibao , asa mdada au mkaka aliyesimama karibu yako amevaa nguo inayoacha makwapa yake wazi , kwa sababu ya joto kwapa inatoa maji na maji yale yana kunakudondokea utajihisije ? nimeuliza hivi maana wengi wakigusia mavazi yasiyofaa watu wanakimbilia kufikiria matamanio ya sex , binafsi nafikiri kuna sababu ya watu kujirejesha kwenye mavazi yenye staha.