Mkuu wa wilaya ya Temeke aamlisha watakavaa nusu uchi wachapwe viboko hadharani

Mkuu wa wilaya ya Temeke aamlisha watakavaa nusu uchi wachapwe viboko hadharani

Source majira

Katika hari inayoelekea kujitungia sheria kulingana na matwakwa ya pande anayoamini yeye either kwa kushauriwa au kwa matakwa binafsi mkuu wa Wilaya Ya Temeke bi Sofia kaamuru maafisa wa vitongoji na wazee wote kuwatandika viboko wale wote watakao vaa nguo amabazo kaziita "nusu uchi" wakati wowote ili kulinda maadili ya kitanzania hasa kwa vijana.

Wazo langu
Hiyo imeanza Temeke tungojee na watawala wa mikoa mingine

Haya ndiyo matatizo ya VIONGOZI kujibadilli kuwa WATAWALA! Yaani wanakuwa kama wafalme; analotaka (hata kama haiangalii ukweli wa hali na matakwa ya waliowengi) inakuwa tuu!

Kuna siku tusishangae kusikia hawa WATAWALA wakitamka WATU WENYE VIPARA WASIBEBE VITU KICHWANI...Ujinga mtupu!
 
uhuru bila mipaka ni utumwa.Huyu amepandwa na jazba tu kuwa mwanae anayo tabia ya kukaa uchi.Lakini,kimsingi ni kauli njema na mashiko yake ila tatizo kubwa ni mapokeo.Hakuna kiongozi wa ngazi ya juu mwenye fikra za kukemea upuuzi huu.Tumewapa madaraka na mamlaka hawayatumii,tutawatwanga wao.Upuuzi mtupu.
 
Upuuzi huu kila mtu ana hoice ziheshimiwe.. Kama ni sheri za mavaz ziwekwe maofisini labda ila kujadili hii ni upuuzi yapo mambo mengi ya maendeleo tuyajadili hayo.. Wilaya yake ina maji? Ama ndio ameona mavazi ndio jambo la maana? Watz km hali ndo hii safari bado mbichi
 
Ndiyo mahakama ya kadhi imeanza?sasa hii naona ni sharia inaanza kuingia taratibu kwa baadhi ya wilaya!kama serikali haitakemea kauli hii tutegemee wilaya zingine nazo kutunga sheria za hovyo zinazopingana na katiba ,kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama zaidi ya hapo ni kujichukulia sheria mikononi!siungi mkononi nguo za ajabu kuvaliwa napinga njia iliyopendekezwa kutatua tatizo.
 
huyu mkuu wa wilaya anapingana na bosi wale, hakusikia juzi siku ya sheria jk alisema nini?? yeye kwa mtazamo wake anaona viboko vinaweza kumaliza hilo tatizo? vipi matatizo ya afya na usafi wa mazingira na elimu katika wilaya yake ameyapa vipao mbele kama hili??
 
Ni uamuzi wa hatari sana!utawala wa sheria unaohubiriwa uko wapi?

Utamshangaa huyo huyo mkuu wa wilaya siku wananchi wakimtia kiberiti kibaka ataanza kusema kwamba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi!! Kweli viongozi tunao nchi hii!!!
 
Huyu mama kalewa madaraka . Badala ya kuimarisha huduma za afya na usafi wa mazingira yeye anataka kupigavwatu bakora huu ni ulimbukeni
 
Hiyo safi sana, ila agizo hilo lisilenge akina dada tu pia wanaume wanaovaa suruali au kaptula huku makalio yakiwa nje washughulikiwe. Inatia kinyaa sana jitu linatembea barabarani huku likionyesha boxer yake chafu eti fashion, pumbavu zenu wavaa kata K wote!
Source majira

Katika hari inayoelekea kujitungia sheria kulingana na matwakwa ya pande anayoamini yeye either kwa kushauriwa au kwa matakwa binafsi mkuu wa Wilaya Ya Temeke bi Sofia kaamuru maafisa wa vitongoji na wazee wote kuwatandika viboko wale wote watakao vaa nguo amabazo kaziita "nusu uchi" wakati wowote ili kulinda maadili ya kitanzania hasa kwa vijana.

Wazo langu
Hiyo imeanza Temeke tungojee na watawala wa mikoa mingine
 
Hata mia ilianza na moja. Mi namuunga mkono 100% kwasababu imekuwa kero na hapa hili sio suala la imani bali maadili tu. Hivi kwenye zile video za maisha ya Yesu wanawake wanavaa vimini? Hii inaonesha wazi kuwa sasa maadili yamevurugwa sio wakristo au waislam hapa kilichopo ni wote tulisimamie hili.

Tunapozungumzia maadili hapo dini weka pembeni kwakuwa hakuna dini inayokubaliana na upuuzi kama huu. Hebu fikiri;unamkuta dada kavaa kinguo mabega na makwapa yako nje pamoja na kitovu.

Sketi ya kuana na ipo kwenye magoti. Jamani mifano mibaya ni mingi mno. Kwa mifano hii je kuna dini inafundisha waumini wake wavae upuuzi huu? Jibu ni hapana,kwahiyo upuuzi huu wa kuiga kutoka ulaya lazima tuupige vita.

Tatizo ni utekelezaji wa hicho alichokitaja, kwani hakuna sheria inayokataza uvaaji huo, wanapaswa kutunga sheria zao kwenye manispaa yao, sasa ukisema mtu achapwe tu viboko... je anachapwa na nani.. Kama ni mtaani je achapwe tu na raia!.. Lazima kuwe na sheria wasije wakamchapa hata kichaa... Kwa sababu watu wakiruhusiwa kuwachapa watu mitaani tu sijui itakuwaje..! Ni lazima zitungwe sheria ndogo ndogo za halimashauri husika ili kufanikisha hili. Viongozi waache kukurupuka!.. Kuna siku wataleta maafa.
 
Ni mtu asiyefahamu nini maana ya utawala bora!Analeta jazba zisizokuwa na maana!
 
Napenda kuuliza maadili ya ki-Tanzania ni yepi? Tanzania tunayo makabila 120 je maadili ya kitanzania ni ya kabila gani? Anazungumzia kuvaa... kila kabila lina uvaaji wake, apite mitaa ya Singida kuelekea Tabora kuna kabila ambalo wanawake hawavai kabisa kitu juu yaani ni kijisketi tu... je hao sio wa-Tanzania.

Naomba huyo mkuu wa wilaya afuate mambo yaliyopo kwenye JD yake aachane na mambo ya mavazi. Kuna maeneo maalum ya kupanga aina ya mavazi sio kila pahali ndio maana ya Uhuru.

Jamaa ametoa mfano wa enzi za Yesu... enzi hizo m-Tanzania ulikuwa unavaa nini? Hata kitambaa ulikuwa unakijua. Nenda Israel ya sasa uone kama wanavaa robs... hadi askari wao wanapiga mlegezo... huo ndio uhalisia...

Mnatakiwa kuwa na mawazo yanayobadilika... kwani kimini chake wewe kinakuhusu nini? Shinda tamaa yako. Huko uarabuni wanakojitanda na kuacha sura ndio ubakaji uko juu kulinganisha na maeneo wanayovaa huru.

Napinga hoja ya kuchapa viboko 100/100.
 
Huwezi kumkamata mnywaji wa gongo alafu akamwacha mpishi aendelee kupika unategemea nini kwahiyo angedili ya maduka yanayo uzanguo za namna hiyo kwanza
 
Yaani mkuu wa Wilaya ndiyo anaona hilo la nusu uchi? Na madangulo ya pale TEMEKE hosptal je, Sugar ray, Buguruni? si zaidi ya nguo fupi? tena pale TEMEKE ni karibu kabisa na Kituo kikubwa cha polisi chang'ombe, waache usanii. akakamate kwanza wale akina dada wa kihaya wanaojiuza usiku na mchana wakiwa nusu uchi mchana na uchi usiku.
 
Na wanaotenda matendo kinyume cha maadili ya taifa wafanyweje? Mkuu wa wilaya ni nani ktk nchi hadi aingilie haki binafsi za mtu binafsi kama za nguo gani uvae? Baadaye atasema wanaokula baadhi ya vyakula ambavyo ni kinyumbe na maadili ya kitanzania. Hii ni hatari sana kwa nchi.
 
Mbona naye huvaa uchi anapokuwa dodoma. Ni uongozi usiofaa, anafahamika sana si mwadilifu
 
Huwezi kumkamata mnywaji wa gongo alafu akamwacha mpishi aendelee kupika unategemea nini kwahiyo angedili ya maduka yanayo uzanguo za namna hiyo kwanza

Wangefunga maduka yanayouza hizo nguo na awe anazikagua nguo zote zinazoingizwa nchini.
 
Hajui atendendalo. Yeye awe polisi, mahakama na magereza. Hawa ndio wakuu wa wilaya na mikoa waliopo. Unatarajia kupata maendeleo kweli?
Sina uhakika aliokotwa wapi kabla ya kuzawadiwa ukuu wa wilaya.

.
Safi sana. Haya mikina dada imezidi mno. Ni hatari hata kwa afya hasa kwa wapanda dala dala wana asilimia kubwa kuambukiza magonjwa ya ngozi za hawa wavaa nusu uchu. Kikwapa nacho ndo usiseme. Shame on you wanadada umliokufa dhamira.
.
 
Back
Top Bottom