Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegele aja na Temeke Gulio-Soko la Makangarawe limekamilika

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegele aja na Temeke Gulio-Soko la Makangarawe limekamilika

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
MKUU WA WILAYA WA TEMEKE MHE JOKATE MWEGELO AJA NA TEMEKE GULIO - SOKO LA MAKANGARAWE LAKAMILIKA

Rasmi sasa Tarehe 19/11/2021 ndani ya Soko Letu La Makangarawe WanaTemeke tunaenda kuandika Historia kwa namna ambavyo wafanyabiashara wadogo wadogo walivyoitikia wito wa kuhama maeneo yote yasiyo rasmi na kuhamia katika maeneo maalumu waliyopangiwa na serikali.

Kutokana na hali hiyo tumewaletea Temeke Gulio kwaajili ya kuendelea kuyatangaza hayo maeneo na kuzitangaza biashara zetu Duniani Kote.

Temeke Gulio litapita na kufanyika kwenye masoko na maeneo maalum yaliyotengwa kwaajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo na si kwingineko.

TemekeGulio litatoa fursa mbalimbali kama ;
📌Kutangaza biashara zetu
📌Kutangaza Masoko/Maeneo yetu ya Biashara
📌Kutoa Elimu ya Fedha na Mikopo nafuu kutoka taasisi mbalimbali za fedha na Manispaa Yetu
📌Elimu Ya Kidigitali jinsi tunavyoweza tumia TEHAMA kuboresha biashara zetu na kujitangaza zaidi
📌Upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu
📌Itakuwa ni fursa ya kutatuliwa KERO na Kupata Elimu juu ya HUDUMA kutoka taasisi tofauti za SERIKALI kama NIDA, RITA,

TANESCO, TRA, DAWASA, Idara zetu za Manispaa n.k
📌📌📌 Kubwa zaidi Temeke Gulio yetu itakuwa live kabisa kupitia Wasafi FM na Wasafi TV ndani ya DSTV Tanzania ni wakati wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa temeke kujulikana Kimataifa.

Shukrani za kipekee ziende kwa Wasafi Media kwa kuwa sehemu ya hili jambo la Kihistoria hasa kwa OFA ya kuzitangaza bure biashara za wafanyabiashara wadogo wadogo wa Temeke kupitia Temeke Gulio.

Pia niwashukuru sana DSTV Tanzania kwa kutuunga mkono katika kufanikisha jambo hili kupitia Kufurushi chao cha Dstv Poa Zigo Kama Lote.

Nawakaribisha Wote Tushirikiane kwenye Temeke Gulio na Mwisho Kabisa Temeke Tukutane Sokoni 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿


FEJscVCX0AIXnx9.jpg
 
Back
Top Bottom