Mkuu wa wilaya ya Ubungo ajitafakari uwezo wake ni mdogo sana

Mkuu wa wilaya ya Ubungo ajitafakari uwezo wake ni mdogo sana

Kuna CCM mwenye uwezo mkubwa wa chochote zaidi ya ujinga?

Sijui hata jina lake ila ndani ya siku chache ametoa pasi mkaa au boko za kutilia shaka uwezo wake.
Alianza na kamata kamata ya machangudoa pale riverside,kesi iko mahakamani ,anaitia serikali hasara maana kesi za ukahaba ni kama za uchawi ,hazina ushahidi wa moja kwa moja,mwisho wa siku wataachiwa tu.

Akaja kumtia korokoroni mwandishi wa The Guardia aliyepiga picha wanafunzi wanaosomea chini ya mwembe.

Hatujakaa sawa akaishia kuzomewa na machinga wa simu 2000 kwa kutilia shaka uwezo wake.

Huyu atumbuliwe tu hafai
 
Wenye akili wako mtaani wanatafuta ajira, na wasio na uwezo ndio hao wenye madaraka..
 
Kwa kweli huyu DC kila nikimuona anaongea kwenye media, ninashawishika kusema uwezo wake ni mdogo sana hasa kwenye mbinu za utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Mara ya kwanza nilimuona akizungumza kwenye tukio moja la wananchi kukosa maji safi kwa muda mrefu. Badala ya kusimama kama kiongozi na kusema nini atafanya, aliishia 'kuwakaanga' watendaji wa DAWASA.

Tukio la pili limetokea hapohapo kwenye ofisi yake ambapo ilionekana vijana wanaotaka kujiunga na vyuo wanapata changamoto kupata namba za NIDA. Ofisi za NIDA zipo hapohapo kwenye jengo la DC. DC naye analalamika kuwa watendaji wa NIDA wanachelewa kuingia kazini.

Sasa DC analalamika huku changamoto anaiona na inatokea kwenye ofisi yake. Ila anasubiri hadi media zifike ndio aseme badala ya kuchukua hatua kabla hali haijawa mbaya.

Katika matukio yote, mawaziri husika ndio walifika na kutoa maelekezo. Sasa huyu DC kazi yake ni nini!

Hii wilaya ina changamoto nyingi tu hasa za miundombinu ya barabara. Kwa sasa mvua zimeisha, badala ya kupambana na hii changamoto, yeye anakimbizana na dadapoa.

Wilaya hii itasubiri sana kwenye suala la maendeleo.
 
Back
Top Bottom