Mkuu wa wilaya ya Ubungo ajitafakari uwezo wake ni mdogo sana

Kuna CCM mwenye uwezo mkubwa wa chochote zaidi ya ujinga?

 

Wenye akili wako mtaani wanatafuta ajira, na wasio na uwezo ndio hao wenye madaraka..
 
Kwa kweli huyu DC kila nikimuona anaongea kwenye media, ninashawishika kusema uwezo wake ni mdogo sana hasa kwenye mbinu za utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Mara ya kwanza nilimuona akizungumza kwenye tukio moja la wananchi kukosa maji safi kwa muda mrefu. Badala ya kusimama kama kiongozi na kusema nini atafanya, aliishia 'kuwakaanga' watendaji wa DAWASA.

Tukio la pili limetokea hapohapo kwenye ofisi yake ambapo ilionekana vijana wanaotaka kujiunga na vyuo wanapata changamoto kupata namba za NIDA. Ofisi za NIDA zipo hapohapo kwenye jengo la DC. DC naye analalamika kuwa watendaji wa NIDA wanachelewa kuingia kazini.

Sasa DC analalamika huku changamoto anaiona na inatokea kwenye ofisi yake. Ila anasubiri hadi media zifike ndio aseme badala ya kuchukua hatua kabla hali haijawa mbaya.

Katika matukio yote, mawaziri husika ndio walifika na kutoa maelekezo. Sasa huyu DC kazi yake ni nini!

Hii wilaya ina changamoto nyingi tu hasa za miundombinu ya barabara. Kwa sasa mvua zimeisha, badala ya kupambana na hii changamoto, yeye anakimbizana na dadapoa.

Wilaya hii itasubiri sana kwenye suala la maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…