UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Katika kukabiliana na uhaba mkubwa wa maji safi na salama unaoikumba Kata ya Mkwajuni pamoja na kata nyingine za Saza na Mwambani wilayani Songwe, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mkwajuni (MKUWASA) kwa sasa inatekeleza mpango haraka wa kuongeza upatikanaji wa maji kupitia mradi wa utanuzi na uboreshaji wa huduma ya maji unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.046.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Amedeus Kisaka, mradi huo unahusisha upanuzi wa mtandao wa mabomba, ununuzi wa mashine za kusukuma maji, pamoja na uchimbaji na uboreshaji wa visima vitano katika kata za Mkwajuni, Saza na Mwambani.
Kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha Sheria Namba 5 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2019, Mamlaka za maji zinawajibika kupanga, kutekeleza na kusimamia miradi ya maji kwa ufanisi.
MKUWASA tayari imeandaa mipango ya muda wa kati na muda mrefu ili kukabiliana na changamoto ya vyanzo vichache vya maji, ikiwemo kuchimba visima vikubwa zaidi na kuongeza uwezo wa visima vilivyopo ili kuongeza uzalishaji wa maji.
Mhandisi Amedeus Kisaka anaeleza kuhusu mipango iliyopo kwa sasa:
Mhandisi Amedeus Kisaka:
"Sisi kama mamlaka tuna mipango wetu madhubuti. Hata mradi huu tunavyoutkeleza ni suluhisho la muda mfupi kwanza. Baada ya hapo tuna mipango ya kati. Mipango ya kati kama mamlaka tutachimba visima vikubwa na kuweka casing kubwa ili tuweze kutoa maji ya kutosha. Kwa sababu visima vyetu vingi vilivyokuwepo hapa vinatubana kwa maana zile... kweli kisima unakuta kimekwenda kina kuanzia mita 120 mpaka mita 150, 160, lakini unakuta vimebana wa casing.
Kwa hiyo mipango wetu ya kati kama mamlaka, tuna mpango tuongeze zile... vile vipenyo vya vile visima, ili tuweze kuweka pampu kubwa, kwa sababu kuna baadhi ya maeneo yana maji mengi. Kama eneo la Kalungu, kisima casing ni nchi 6, lakini yield capacity, yaani uwezo wa kisima, lita 25,000 kwa saa. Mipangilio ina uwezo wa kuchukua lita kama 20,000, almost 80% of that. Lakini kisima kina casing ndogo siwezi kuweka pampu... kuongeza pampu pale tukaweka pampu kubwa zaidi.
Tuna mpango eneo la Saza, eneo la Saza kuna maji mengi. Tumeshainitialize yale maeneo tutachimba visima vingine vikubwa, halafu tujenge matanki mengine makubwa ya ambaye matanki hayo yawe iwanda wa juu, maeneo ya Patamela kule na maeneo ya Mimbini. Yale matanki yatakuwa na uwezo wa kuleta maji na maeneo ya Saza na hata kurudisha mpaka Mkwajuni. Kwa hiyo hiyo ni suluhisho la kati.
Halafu kuna mipango ya muda mrefu ya plan zetu. Tumeshaanza kuainisha sasa tuangalie mito ile mikubwa. Kwa mfano kama kuna Mto Luika. Mto Luika tumeshazungumza na tumeshapata data zake walishatupa ndugu zetu wale wa mabonde kwa ajili ya kufanya uwekezaji mkubwa kwenye ile mito. Hiyo ni mipango ya muda mrefu kwa sababu tunatambua kwamba leo Mkwajuni ya leo sio ya kesho, kwa maana watu watazidi kuongezeka, mahitaji yatazidi kuongezeka na nanyi mnatambua kwamba huku kuna shughuli za madini. Kila siku kila kukicha watu wanazidi kuhamia."
Hata hivyo, wakati serikali ikieleza mipango yake, wananchi wa Mkwajuni wanasema wanahitaji kuona hatua za vitendo zaidi zikifanyika badala ya ahadi pekee. Fredrick Vungwa, mkazi wa kata hiyo, anasema tatizo la maji limekuwa la muda mrefu huku miradi mingi ikichelewa kukamilika, na hivyo ana wasiwasi kama mradi unaotekelezwa kwa sasa utakamilika kwa wakati.
Fredrick Vungwa (Mwananchi):
"Chanzo cha maji ambacho Mheshimiwa Rais... Rais wa Jamhuri ya Muungano, mama wetu Samia ametoa pesa bilioni 4 kwa ajili ya kukomesha hii adha ya ukosefu wa maji. Sasa tunachojiuliza sisi kwamba kila tunapokuwa tunaahidiwa, haya mambo hayafanyiki kwa wakati.
Ni kweli tunaona mtaani mabomba yanatandikwa, lakini ile shughuli mimi sina imani itakuwa bado tutasongeza siku za mbeleni. Sasa sisi tunapenda kama jambo au kama mradi unafanyika ni wa kuchukua muda mrefu, lugha zisiwe zile za kufupisha, eh, kwamba bwana hii kesho kutwa mradi utakuwa hewani, maji haya ya mvua yameanza kutoka, lakini sio ya kuyategemea sana."
Shaibu Kapingu ni Diwani wa Kata ya Mkwajuni, anaeleza kuwa bado ana matumaini makubwa na kwamba hadi kufikia mwaka 2030, tatizo la maji katika eneo la Mkwajuni litakuwa limepungua kwa kiasi kikubwa.
Shaibu Kapingu:
"Kwanza nakiri, shida ya maji ipo. Yaani mimi kama kiongozi siwezi kusema hakuna shida ya maji, hapana. Shida ya maji ipo. 2030 ninatamani wananchi waje waniulize kuhusu maji. Na mimi nitakuwa na majibu ya kuwajibu kuhusu maji. Na kihistoria ndugu mtangazaji, mimi wakati naingia mwaka 2020 nilikuta kaya 100 ndizo zimevuta maji majumbani. Leo tunavyozungumza kwenye kata yetu kaya zaidi ya 6,000 zimevuta maji."
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Fadhili Nkulu amesema mipango ya muda wa kati na mrefu ya kuongeza huduma ya maji katika Kata ya Mkwajuni na Wilaya ya Songwe kwa ujumla, iliyobainishwa na Mkurugenzi wa Maji, itakwenda sambamba na uongezekaji wa huduma ya nishati ya umeme kwa ajili ya kusukuma mitambo ya maji ili iweze kuwafikia wananchi kwa wakati.
Fadhili Nkulu (DC Songwe):
"Sisi tunatumia line inayotokea Mbozi. Mbozi inalisha Ijeje, inalisha Tunduma, inalisha wapi... ile line imezidiwa tayari. Kwa hiyo, mpaka umeme uje ufike huku, mara nyingi hapa njiani unakatika. Lakini ziko solution ambazo zimefanyika jitihada za makusudi. Yuko mradi ambao ndio utakuwa solution kubwa wa utafutaji wa umeme mkubwa kwenye msongo kV 220 ambao unatoka Iganjo, Mbeya kuja kwenye substation itakayojengwa hapa Saza. Huu umeme unaweza kuzalisha MW 72, na uhitaji wetu hapa kwa wilaya ni 25.4. Kwa hiyo unaweza kuona kwamba tutakuwa na ziada ya umeme.
Na huu mradi naokwambia utekelezaji wake utaanza baada ya wananchi kuridhia maeneo yao ili miundombinu iweze kufanyika, na solution itakuwa imepatikana. Vyanzo vyetu vya maji hapa kwenye kwa wenzetu wa Mamlaka ya Maji Mkuwasa ni visima ambavyo visima vinatumia pump, na pump hizi zinatumia umeme. Kwa hiyo umeme unapokuwa umekatika, there is no way huwezi kupump yale maji. Kwa hiyo hii mambo yanategemeana sana. Ukikosa umeme utakosa na maji."
Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa mwaka 2025, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Kundo Mathew, alitembelea na kukagua mradi wa maji unaotekelezwa kwa sasa, na kuahidi kushughulikia tatizo la fedha zilizocheleweshwa ili mradi huo uendelee, pamoja na kuzagiza bodi za mabonde ya maji nchini kufanya tathmini ya kina ya vyanzo vyote vya maji, hatua itakayoiwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za kupanga mipango ya sasa na ya baadaye.
Mhandisi Kundo Mathew (Naibu Waziri):
"Cha kwanza, tufanye tathmini ya vyanzo vyetu vyote vya maji. Tujiridhishe kama kuna uvamizi, kama kuna uharibifu, na kama kuna mabadiliko ya tabianchi ambayo yameathiri vyanzo vyetu vya maji, kama vimekauka, ili tuwe na takwimu sahihi ya vyanzo ambavyo vinafanya kazi. Lakini pia tuweze kubaini na kuibua vyanzo vingine vipya.
Kama serikali, ni lazima tuwe na database ambayo ina updated taarifa za vyanzo vyetu vya nini? Vya maji, na hali ya vyanzo ilivyo. Kwa sababu chanzo cha maji hakikauki siku moja, kunakuwa na tabia na mwelekeo ambao unaonyesha kwamba hiki chanzo kinaanza kutuacha. Kwa hiyo ni lazima kama serikali tuwe na taarifa ambazo zinatuonyesha kwamba hali halisi tunakoelekea ikoje."
Kwa sasa matumaini ya wananchi wa Mkwajuni yameelekezwa kwenye mradi unaotekelezwa, huku wakisisitiza uamuzi wa serikali kuchukua hatua za haraka, kuongeza uwazi katika utekelezaji wa miradi ya maji, na kuhakikisha suluhisho la kudumu linapatikana ili kulinda afya, uchumi na ustawi wa jamii kwa ujumla.
ANDIKO LA: Heneliko Malo
Makala imeandaliwa na Mwandishi anayeshiriki katika programu maalum ya kukuza uandishi wa maslahi kwa umma (Public Interest Journalism Fellowship) inayoratibiwa na UTPC kwa kushirikiana na IMS