Mkwasa anapwaya ukocha timu ya taifa.

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Nimekuwa najiuliza taratibu zilizomfanya Charles Boniface Mkwasa kuchaguliwa kuifundisha timu ya soka ya taifa letu kama zilikidhi nia yetu ya kusonga mbele, naambulia kusononeka tu. Kocha huyu anafanya mambo kama anashinikizwa vile na kwa sasa anazidiwa kimaarifa na kina Mbwana Samata na Tomas Ulimwengu. Juzi kataja kikosi na kukiita kambini jana kaahirisha kambi eti vilabu vinajiandaa kwa ligi! TFF tafuteni kocha mwengine wa timu hii.
 
Maandalizi sio tu timu ya Taifa ila kuanzia penye vilabu vyetu je tunao hao wachezaji? Kocha wa taifa anakaa nao wiki mbili je huko vilabuni tunawalea vipi wachezaji wetu? Kuna hawa wawili mungu awa rehemu stiven kashi na shaibu amadou wa nigeria mbona walikuwa na rekodi nzuri tu.
 
Mechi hii inatakiwa tusicheze haina maana yeyote. Serilali inabana matumizi je waziri husika halioni hili hapa pesa itapotea bure. pia kocha mkwasa kwa bahati mbaya alishindwa urefu wa twiga je wa mlima kilimanjaro urefu wake ata uweza. Tutafakari tuchukue hatua.
 
Tumeshakuwa na makocha wageni wengi tu na hakuna sehemu nzuri tunayoweza kujivunia kuwa wametufikisha, mkwasa anaweza kuwa chaguzi sahihi tumpeni muda tu, kwanza ata record yake ninzuri ata ukifanya comparison na makocha waliopita, apewe muda kwanza nyie wenyewe mnajua wabongo walivyo wagumu kuelewa so tuwaachie huyu huyu mzawa anajua hadi kimakonde
 
Mkuu, hao wana rekodi kumzidi wa kwetu.
 
Dhana ya uzawa tukiiendekeza hatufiki popote.
 
Mkuu, hao wana rekodi kumzidi wa kwetu.
Ni kweli ila walianzaje? ni kwamba lazima kwanza tuwe na wachezaji wa kimataifa au nusu ya hapo sidhani kama duniani kuna nchi ilifanikiwa bila kuwa na wachezaji wenye kiwango fulani hapo ndipo pa kuanzia. Ukisema dhana ya uzawa inatudondosha leo chagua world class kocha mpe timu yetu kama hatutamtimua.
 
Anajaza mafowadi wa Yanga ambao husugua benchi kila siku. Namba zao wanazo ma pro. Hii ni hujuma kwa Taifa.
 
Anajaza mafowadi wa Yanga ambao husugua benchi kila siku. Namba zao wanazo ma pro. Hii ni hujuma kwa Taifa.
Huu ndio uchawi, ufitini na ujuha.... Kuna forward wa Yanga aliyecheza timu ya Taifa au hata kuitwa tu kipindi cha ukocha wa mkwassa!!???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…