Mkwasa: Tatizo sio wachezaji tatizo uwanja ulikuwa na koki za maji

Mkwasa: Tatizo sio wachezaji tatizo uwanja ulikuwa na koki za maji

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Kocha wa Kilimanjaros stars amedai tatizo kubwa la timu yake kupoteza ni hujuma walizofanyiwa na Algeria moja wapo ni kuwepo kwa koki za maji uwanjani (pitch).

Walifanya michezo hii kwenye upande stars na kubadilisha tena koki kufuata upande wa stars kwenye second half.

Nini maoni yako mwana michezo mwenzangu?
 
halafu wao algeria walikuwa wakifika goli lenye maji wanafungaje? kama waliona hivyo kwanini hawakuvaa viatu vya kuzuia kuteleza kipindi cha pili? waongee na jecha awasaidie kufuta matokeo
 
Mkwasaaaa, tukubali tu Algeria wako mbele sana zaidi yetu, koki zilifanyaje kazi kuwasaidia wao?
 
Hivi Mkwasa bado ataendelea kulipwa sh. milioni 25 kwa mwezi? Nauliza tu
 
Kujiuzulu sio kwamba umeshindwa bali ni kujenga mazingira ya uwajibikaji kwa siku za mbeleni.
Sasa hizo koki mbona sisi hatukuwawekea walivyokuja hapa, au kuna asiyejua fitina za timu za Kaskazini!?
Kumbuka wengi waliangalia mchezo wa kwanza Dar es Salaam na timu yetu ilicheza vizuri tu, kasoro ikawa ni kushindwa kutumia nafasi tulizopata na mbaya zaidi tulivyoruhusu magoli mawili (kizembe).
Angelitolea hivyo ufafanuzi tungemuelewa lakini mambo ya koki ni uzushi. Kocha mzuri lakini katufungisha goli 7 ambayo ni aibu!
 
mbongo ukimpa nafasi ya kujitetea tu anakuacha.

sasa baada ya kugundua koki za maji why nao wasitumie fursa kuwafunga algeria
 
Akubali tu kwamba algeria walituzid na hatuwawez
Sisi kiwango chetu ni ile algeria tuliyocheza nayo dsm sio ile ya ulayaulaya tuliyocheza nayo algeria
 
Hata ile free kick iliingia sababu ya koki ya maji? Na zile set pieces nazo? Ahaaa! Tusifiche maradhi!
 
Access denied in this thread, kwa nini?. Kitufe cha LIKE kimegoma kabisa@Invisible
 
Kocha wa Kilimanjaros stars amedai tatizo kubwa la timu yake kupoteza ni hujuma walizofanyiwa na Algeria moja wapo ni kuwepo kwa koki za maji uwanjani (pitch).

Walifanya michezo hii kwenye upande stars na kubadilisha tena koki kufuata upande wa stars kwenye second half.

Nini maoni yako mwana michezo mwenzangu?

kwaiyo star walizuiwa kucheza upande mwingine wa uwanja!
 
Kocha wa Kilimanjaros stars amedai tatizo kubwa la timu yake kupoteza ni hujuma walizofanyiwa na Algeria moja wapo ni kuwepo kwa koki za maji uwanjani (pitch).

Walifanya michezo hii kwenye upande stars na kubadilisha tena koki kufuata upande wa stars kwenye second half.

Nini maoni yako mwana michezo mwenzangu?

Mkwasa ni kocha wa Timu ya Tanzania (Taifa Stars)

Kibadeni ni kocha wa Timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars)
 
Akubali tu kwamba algeria walituzid na hatuwawez
Sisi kiwango chetu ni ile algeria tuliyocheza nayo dsm sio ile ya ulayaulaya tuliyocheza nayo algeria

Wajamaa walitusoma mbinu zetu na wakazifanyia Kazi

Wakaita wachezaji wao ambao mechi ya kwanza ya Dar es salaam awakuwepo, wakamaliza shughuli mapema,

Tusitafute mchawi, tutengeneze shule za mpira kwa wingi, matunda yataonekana tu..
 
Changamoto nyingine ktk nchi hii ni hii: KUBADILI KAZI YA MSINGI YA UBONGO
 
Back
Top Bottom