Ilianza mwaka 2000 ambapo tayari huyu Bwana alikuwa tayari ameshafilisi viwanda vyetu vya ngozi, tayari alishategeneza himaya yake ya kisiasa ndani ya CCM na kuitumia kuhakikisha kampuni yake ya Caspian inapata kandarasi serikali. Na kampuni hii ndio yenye mahisa humo vodacom. Lakini alikuwa pia na makampuni mengine pembeni yaliyokwiba fedha za mfuko wa Japan. Na pia lile kampuni lake lingine lililojibebea fedha za import support. Halafu akaendeleza mtaji wake miaka ya 2002-2006 kwa kutumia mafedha mengine ya BOT. Huyu ndiye Kagoda ninayemfahamu! Sasa ni bilionere, hata mkimchanganya vodacom, mkono wake upo kila mahali. Upo TICS, msuse kuingiza makontena. Upo habari corporation, msuse kusoma rai na mtanzania. Upo Mwananchi, nako pia msuse. Lakini upo pia ndani ya CCM, hisa zake huko ni nyingi zaidi. Mkitaka kumkomoa basi mjitoe kwenye Chama Cha Mafisadi(CCM),atabaki tu na vile vitega uchumi vyake vilivyopo Oman, Iran, Maritius etc. Hivi ile tenda ya kujenga kiwanja cha ndege alishakamilisha?
Asha