Mlaani hapa kiongozi aliyekukosea

Mlaani hapa kiongozi aliyekukosea

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mimi naanza.

•Alaaniwe kiongozi aliyeuza nyumba za serikali kwasababu yoyote ile. Nyumba zile ni za watumishi wa kawaida, wakaziuza kisha watumishi wakaanza kuishi kifukara lakini wao wenyewe waliishi nyumba za bure. Watumishi kutokana na vipato vyao hawawezi kupata viwanja vya milioni 30 hivyo wananunua viwanja vya milioni 2 maporini kisha pesa nyingine wanaanzia ujenzi.

Baadaye shida inakuja muda na gharama za kufika kazini . Sababu zao mfu eti ni gharama kuziendesha. Kwani kila nyumba ikifungwa mita ya maji na umeme kisha kila mtumishi ajilipie mwenyewe kuna tatizo?

Service ya rangi ifanywe na mtumishi mwenyewe na ikiwa atahamishwa kwenye nyumba husika ndani ya miaka 3 baada ya kupaka rangi serikali itaangalia namna ya kum refund kidogo na ikiwa ataishi zaidi ya miaka 3 basi hakuna refund.

• Alaaniwe aliyeizika Tanganyika huku Zanzibar ikiendelea kung'ara. Wote waliohusika vizazi vyao vilaaniwe.

•Alaaniwe kiongozi yeyote aliyehusika kuleta kikokotoo cha hovyo na kuzuia fao la kujitoa. Yeye mwenyewe kajitoa nje ya alichokileta kwa watumishi licha ya kukisifia kuwa ni chema
 
Hatakama ni Rais?
Hilo nakuachia wewe. Mimi nasema hivi aliyeuza nyumba za serikali kisha watumishi wenye vipato duni tukitokea mbali na mjini kuelekea mjini kufanya kazi Alaaniwe.

Una nyumba Chanika unafanya kazi Posta. Gharama za usafiri na muda vinatesa sana
 
Hilo nakuachia wewe.
Mimi nasema hivi aliyeuza nyumba za serikali kisha watumishi wenye vipato duni tukitokea mbali na mjini kuelekea mjini kufanya kazi Alaaniwe.
Una nyumba Chanika unafanya kazi Posta. Gharama za usafiri na muda vinatesa sana
Haaaaa kuna landcruiser imepaki nje kwenu haina plate number.
 
Mimi naanza.

•Alaaniwe kiongozi aliyeuza nyumba za serikali kwasababu yoyote ile. Nyumba zile ni za watumishi wa kawaida, wakaziuza kisha watumishi wakaanza kuishi kifukara lakini wao wenyewe waliishi nyumba za bure. Watumishi kutokana na vipato vyao hawawezi kupata viwanja vya milioni 30 hivyo wananunua viwanja vya milioni 2 maporini kisha pesa nyingine wanaanzia ujenzi.

Baadaye shida inakuja muda na gharama za kufika kazini . Sababu zao mfu eti ni gharama kuziendesha. Kwani kila nyumba ikifungwa mita ya maji na umeme kisha kila mtumishi ajilipie mwenyewe kuna tatizo?

Service ya rangi ifanywe na mtumishi mwenyewe na ikiwa atahamishwa kwenye nyumba husika ndani ya miaka 3 baada ya kupaka rangi serikali itaangalia namna ya kum refund kidogo na ikiwa ataishi zaidi ya miaka 3 basi hakuna refund.

• Alaaniwe aliyeizika Tanganyika huku Zanzibar ikiendelea kung'ara. Wote waliohusika vizazi vyao vilaaniwe.

•Alaaniwe kiongozi yeyote aliyehusika kuleta kikokotoo cha hovyo na kuzuia fao la kujitoa. Yeye mwenyewe kajitoa nje ya alichokileta kwa watumishi licha ya kukisifia kuwa ni chema
Aliyeuza nyumba za serikali hadi leo sijaelewa alikuwa na nia gani na nchi hii, yani ukisikia kuuza nchi ndio kule
Wewe umekaa masaki huku kizazi kilichobaki chote kisipate nafasi hiyo milele kwa maamuzi na faida za watu wachache tu kwa ulafi wao
 
Hilo nakuachia wewe. Mimi nasema hivi aliyeuza nyumba za serikali kisha watumishi wenye vipato duni tukitokea mbali na mjini kuelekea mjini kufanya kazi Alaaniwe.

Una nyumba Chanika unafanya kazi Posta. Gharama za usafiri na muda vinatesa sana
Mtu anayejitambua hawezi kuishi chanika
 
Aweso ulaaniwe wewe, unatesa watu na maji. Ni lazima mnafanya biashara na viwanda au ujinga mwingine. Hao wa chini hawana ubavu wa kuzuia maji zaidi ya miezi minne. Amri imetoka kwako. Ulaaniwe, maji ni uhai.
Kwa sababu ni waziri wa maji...basi laana hiyo imeshaingia katika maji....na siku ukiyatumia tu...laana hiyo itakuvaa mwenyewe ilihali maji hayo hayatawaathiri wengine....

Usipende KULAANILAANI hovyo....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Walaaniwe viongozi wote wasiotaka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi......
 
Back
Top Bottom