Mlale pema ndugu, jamaa na mashujaa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Ulale pema bk wa TMK mapanga/
ulale pema Steve 2 k/fadha nelly langa/
ulale pema Albert mangwair/John mjema mapacha/ Ni njia Moja tunayoelekea nitafuata/
ulale pema remmy ongala/ kweli kifo hakina huruma japo foleni msafara/
ulale pema mark 2 b/ mapema umesonga Mr ebbo/
Ulale pema d rock songa/
ulale pema marijani rajabu/
tx mosh/mzee ngurumo buriani babu/Justine kalikawe/haki iko wapi kwa sugu umekwenda leo uko mbali naye/
ulale pema cool James dandu hata uliyempenda pia analia cool James wangu/
ulale pema complex na Vivi/bi. kidude daima nakuombea ulale pema bibi/
ulale pema YP Umetangulia ndo maana nasema RIP/
ulale pema side boy/
Ulale pema my bro pablo/ tutaonana Tena mcee/
Ulale pema Adam kuambiana/ umekwenda tumebakia binadam kuambiana/
Ulale pema pwagu ulale pema pwaguzi/ na sajuki/zikufikie salamu salama.
Ulale pema Rachel haule/ umeondoka mapema wengi wanatamani tena uwe na uwepo/
Ulale pema mwasisi wa vichekesho mzee small ngamba A.K.A baba kapeto/ bila kumsahau mzee majuto.
Ulale pema kanumba/ vema uliitangaza Tanzania uende safari Njema kwa muumba/
Pia ulale pema mzee kipara mengi nimejifunza kwako ulikuwa mzee wa busara/
Ulale pema sharo milionea/ wa muheza tanga kwa muweza Dua bado nakuombea/
Nakukumbuka George Tyson/Mr mlepoloo na Mr John stephano/
Ulale pema maneto/Jose kesi/kwa mola sio kwa shwetani/
Ulale pema Max wa mizengwe/ imetokea Mungu kukupenda Zaid nafsi yako haijapotea/
Ulale pema chuchuru chuchuru mwenga/Nas B/nasibu James mkoba/balterzari/
Ulale pema chacha wangwe/
hayati mwalimu mheshimiwa Julius kambarage/
Ulale pema amina chifupa/
mwende safari njema kwa muumba
Mlale pema ruge/na mzee wa mastori ya town/
Ulale pema baba uliyenizaa bila wewe,mimi ningekuwa Nani kwenye hii mitaa/
Mlale pema ndugu, jamaa na mashujaa
 
Bika ku mmention Masogange,bado haujakamilika
 
Wote hao vifo vyao vilipangwa jinsi walivyokufa pindi tu walipozaliwa
 
Ghetto ambassador huyo ....[emoji110][emoji109]
 
"Refiki WA kweli"

By langa ulale pema peponi


Wanangu jizzo walikupiga wakakuua, fuvu, kinyaa, omy boy walikuchoma moto ila hawajui mwizi pia nae ni binadamu ulale pema blood mwamba , haruna maspaki wa manzese ulifia gerezani kwa kipindupindu tumekuwa wote mlale pema tutakutana tena paradisoo

Bila kumsahau mwanangu wa faida chedi mapenzi yalikuua ila sema nini wana tukikutana paradisoo kutanoga Sana


Mwanzo mwisho tutalipiga singeli na lile goma la "mchumba mbona utokei mamiloo" "nakuja!!" mwenzako nimemiss shoo


[emoji17] [emoji17] [emoji22]

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Huyo nas b aliyetajwa ni yupi? Au ni yuleambaye kwenye nyimno zake husema nas b nas bizinez?
 
“Mshike mshike ndege tunduni”.

Yule jamaa aliyefungua verse ya kwanza alifanya unyama sana, badae kaamua kupumzika kwa amani mchizi.

Ni nani anajua jina lake? ALALE pema.

Jamaa alijipatia shabiki wa bure hapa sema ndo sikumsikia tena popote, aaaah Walter verse haijaishaaaa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…