Mlela: Ninapenda maisha ya kiki

Mlela: Ninapenda maisha ya kiki

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
692
Reaction score
880

pic+mlela.jpg

Yusuph Mlela

Dar es Salaam. Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania, Yusuph Mlela amesema anapenda maisha ya kiki, kwamba kila analolifanya katika jamii ni kwa ajili ya kiki.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Agosti 27, 2019 baada ya kuulizwa na Mwananchi kama kabla ya kufanya jambo lolote hupenda kutanguliza kiki ili jambo husika liweze kuteka vichwa vya mashabiki wa filamu nchini.

“Niseme tu ukweli napenda kiki, watu wanaonizunguka waelewe kila kitu ninachofanya ambacho kinakuwa na gumzo wajue ni kiki, kwa sababu najua kiki ndio huwafanya watu wawe na umakini wa kukufuatilia kabla ya kutaka kufanya kitu,” amesema Mlela.

Kauli ya Mlela imekuja siku chache baada ya kuibuka mjadala mtandaoni kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Anna Exavery maarufu Ebitoke.

"Suala la Ebitoke na mimi kama ni kiki au wapenzi nitakuja kulizungumzia, kwa sasa siwezi kusema ni kiki au sio kiki,” amesema Mlela

Chanzo:Mwananchi
 
Kitu cha ajabu sijaona huyu mwamba akimposti yule demu,,kila mara ni ebitoke tu ndo anaposti halafu hii kama itakua couple anayefaidika zaidi ni Mlela maana tulishamsahau lakini hii couple imemuibua.
 
Kindege ndege [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom