Mlifungua nyuzi kuituhumu Kenya, polisi wenu wanasema lafudhi za Afrika Kusini

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Ashukuriwe Mungu MO amepatikana, polisi wa Tanzania wamesema waliomteka walikua wanaongea kilugha cha Afrika Kusini na pia lafudhi za huko. Sasa mliokua mnafungua nyuzi na kuituhumu Kenya kwamba imehusika ili iwahujumu na kukwamisha sijui SGR yenu au mengine, vipi mtabadilisha wimbo na kuelekeza pua Afrika Kusini au mtawaogopa wale.

Nyie bana na hizi show zenu za Bongo movie.

Kwanza tunashukuru sana kwa kapatikana kwa Moja, lakini hili lisitufanye kuhamaki na kubadilisha uhuru wetu. Kila Mtanzania lazima ajisikie yuko huru nchi kwake.

Lafudhi lugha haina maana yoyote, hata wewe MK254 siku nyingine unaogea na lafudhi ya kihaa ya Kogoma.
 
Wenyewe ndio mumetangaza kwamba lafudhi zilikua za Afrika Kusini kwa kusudi la kuaminisha umma haikua kazi ya Watz kama kwamba hapo ulipo wewe hauwezi ukaiga lafudhi za Kirusi.
 
Nadhani lafudhi haimaniishi kuwa watu hao wametoka huko, wanaweza kutoka kokote, Kenya, Uganda au hata wanaweza kuwa Watanzania wenyewe, kwani hakuna watu wenye uwezo wa kuigiza sauti na lafudhi za wengine? Suala la muhimu ni kuwa amepatikana akiwa hai...
 
Suala la lafudhi limeibuliwa ili kuaminisha haikua Watanzania, ila nijuavyo kwenye movie za utekaji, watekaji huiga sauti na lafudhi.
 
I agree with you. Na kama ni kweli watekaji walitoka South Africa basi tuna shida kubwa katika suala la ulinzi kama nchi, kwa akili ya kawaida tu unaweza kujiuliza: hivi wamewezaje kumrudisha kwa kutumia gari lile lile walilotumia kumteka? Ina maana hawa watu wanajiamini sana?!...

Yaani watekaji hao wakaenda kumtupa Gymkama, karibu na Ikulu bila kujali ulinzi uliopo mahala hapo, huku wakijua wanatafutwa kila kona!...
 
😅😅😅😅ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.
Maudhui ya unafiki nchini tanzagiza
 
Ashukuriwe Mungu MO amepatikana, polisi wa Tanzania wamesema waliomteka walikua wanaongea kilugha cha Afrika Kusini na pia lafudhi za huko. Sasa mliokua mnafungua nyuzi na kuituhumu Kenya kwamba imehusika ili iwahujumu na kukwamisha sijui SGR yenu au mengine, vipi mtabadilisha wimbo na kuelekeza pua Afrika Kusini au mtawaogopa wale.

Nyie bana na hizi show zenu za Bongo movie.

Sasa hivi watafungua nyuzi zinazosema kenya yamuachia mo yaogopa kipigo cha JPM hahahahaha just joking
 
I agree with you. Na kama ni kweli watekaji walitoka South Africa basi tuna shida kubwa katika suala la ulinzi kama nchi, kwa akili ya kawaida tu unaweza kujiuliza: hivi wamewezaje kumrudisha kwa kutumia gari lile lile walilotumia kumteka? Ina maana hawa watu wanajiamini sana?!...

Yaani watekaji hao wakaenda kumtupa Gymkama, karibu na Ikulu bila kujali ulinzi uliopo mahala hapo, huku wakijua wanatafutwa kila kona!...
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Hii nyundo ngumu
 
Watanzania ombeni msamaha kwa kutuharibia jina la si hivyo
 
Ashukuriwe Mungu MO amepatikana, polisi wa Tanzania wamesema waliomteka walikua wanaongea kilugha cha Afrika Kusini na pia lafudhi za huko. Sasa mliokua mnafungua nyuzi na kuituhumu Kenya kwamba imehusika ili iwahujumu na kukwamisha sijui SGR yenu au mengine, vipi mtabadilisha wimbo na kuelekeza pua Afrika Kusini au mtawaogopa wale.

Nyie bana na hizi show zenu za Bongo movie.

MK kumbe hata hao polisi hakuna kitu walichokifanya. Ni hao watekaji nyara waliomuwachilia Mo kwa hiari yao. Kwa hivyo hawa polisi mchango wao ni kama zero tu.
 
Wasiwasi wangu isiwe hao watekaji wamemuachia baada ya kulipwa maana itaanzisha utitiri wa haya matukio.
 
Nadhani lafudhi haimaniishi kuwa watu hao wametoka huko, wanaweza kutoka kokote, Kenya, Uganda au hata wanaweza kuwa Watanzania wenyewe, kwani hakuna watu wenye uwezo wa kuigiza sauti na lafudhi za wengine? Suala la muhimu ni kuwa amepatikana akiwa hai...
Swala la pili muhimu ni kuwa ndeze hawa wakamatwe washitakiwe oops sirikali iikamate sirikali inawezekana kweli?
 
Back
Top Bottom