Hayawi hayawi yamekuwa..........yale yaliyokuwa yakisemwa na Kina Mar. Prof Seth Chachage sasa yanaanza kujionyesha.
Wageni wanaanza kuleta "ubaguzi wa kimatabaka" kwa watanzania.
Jana nilishangaa pale mlinzi wa Mlimani City alipomwambia dereva wa bajaj kwa "Uongozi wa Mlimani City hauruhusu Bajaj kuingia ndani ya eneo la Mlimani City". Maskini dereva asiyejua hili wala lile akwaomba samahani wateja na kuwashusha getini.
Uongozi wa Mlimani City una uwezo gani wakubagua....wanaoendesha bajaj wasiingie ndani ya eneo hilo. Je hawa nao sio watanzania wanaojitafutia riziki na isitoshe bajaj nyingi huingia pale kuleta wateja na kutoka nje.
Naona makaburu sasa wana "export" ile racism yao.
Nilifanikiwa kuongea na dereva mmoja wa bajaj naye akakiri hata wao wanashangaa juu ya uamuzi huu.
Mimi napendekeza iwapo hili litaendelea watanzania tuache kwenda Mlimani City.
Haina maana kwamba anayeingia na saloon car ndiye mwenye uwezo au anayeingia na bajaj ndio hana uwezo. Watanzania tuna uwezo wa kwenda sehemu yoyote mahali popote na kamwe hatujawahi kuwa graded kwa vyombo vya usafiri tunavyovitumia.
Kama kuna tatizo limetokea muhimu hapa ni kuwawekea wenye vyombo vya bajaj utaratibu wa kuingia na kutoka kwenye eneo hilo na sio "kuwazuia kuingia"