Mama Lao, Nadhani unachokiongea hapa kina mantiki.
Lakini kwa maoni yangu..umeendeleza ule ule mtindo wetu watanzania kuona kitu na kulalamika baadaye. wewe ulivyoona dereva wa Bajaji anaambiwa arudie getini, ulichukua hatua gani? kwa vigezo vyangu..mi sikujui lakini kama una uwezo wa kubonyeza keyboard..basi wewe ni middle class au zaidi kwa hiyo hata uelewa wako ni mpana.
Yes, from your story, alichofanyiwa mwenye Bajaji si sawa, lakini hata wewe ulichofanya si sawa. Kwenda kuongea na dereva wa Bajaji kweli ulitegemea nini? Kwanini hukwenda kuwaona wausika moja kwa moja?
Kwa maoni yangu: Ungeenda moja kwa moja ukaomba kumuona meneja wa Mlimani city na kumuuliza kama kuna sheria/utaratibu huo ambao umewekwa na wao. Au ni walinzi waliamua kuweka utaratibu wao. Iam sure huyo meneja angekupa jibu sahihi na wewe baada ya hapo ndo ungefanya conclusion kuwa either kuna ubaguzi au vipi.
So next time ukiona tatizo kama hilo..siyo kuja JF na kumwaga "the dataz za ubaguzi wa makaburu". Do something siyo kulalamika tuu. Huwezi jua hata huyo meneja wa Mlimani City anaweza kuwa hajui walinzi kama wanawanyanyasa watu wa bajaji... Kwa kufanya hivyo, ungekuwa umewasaidia madereva na perhaps yule boss angeona kwamba kuna watu waelewa kwenye nchi yetu ambao wanafuatilia mambo. Na indirectly, ungekuwa umesaidia wengi dhidi ya manyanyaso ya walinzi..
Jamani changes ni initiave zetu wenyewe...Tusipende kulaumu tuu kwa yale ambayo we can influence changes.
Mada yako hapo juu, inaweza kuwa na ukweli, lakini ukiangalia..ni ule ule mwendelezo wa watanzania wa "kupenda kulaumu"
NEXT TIME, DO SOMETHING!
Masanja,