Hata kwenye mabaa yetu ya mtaani wanawazuia machinga sembuse vibatavuzi kuzuiwa
Kwenye jiji la Arusha kwa wale ambao wameshafika sehemu inaitwa Maasai Camp watakuwa wanajua kwamba hamna mtu anayeruhusiwa kuingia pale kwa miguu maana yake lazima uwe na gari ili uweze kuingia na sababu maalun=mu ni kwamba ili kuzuia vibaka na flycatchers ambao still ndio wanaojaza hiyo sehemu ya starehe na vibaka tele!
Mtoa pesa ni kutoka botswana ila ametumia makaburu kuendeleza eneo hilo katika upangishaji na kadhalika , kiko eneo la udsm ila mkataba ni wa miaka 50 ndio itakuwa rasmi mali ya udsm
upo hapo
Unamaana kwa kipindi chote hiki hawa jamaa wanakamua tu mihela na UDSM hawalipwi pango au ardhi wanayo tumia kuchumia kwa miaka hiyo 50?
Duh si mchezo waTZ ndo tulivyo baada ya miaka hiyo 50 si majengo yatakuwa yamesha choka jamaa watakuwa wamepata faida mara dufu...
Mama Lao, Nadhani unachokiongea hapa kina mantiki.
Lakini kwa maoni yangu..umeendeleza ule ule mtindo wetu watanzania kuona kitu na kulalamika baadaye. wewe ulivyoona dereva wa Bajaji anaambiwa arudie getini, ulichukua hatua gani? kwa vigezo vyangu..mi sikujui lakini kama una uwezo wa kubonyeza keyboard..basi wewe ni middle class au zaidi kwa hiyo hata uelewa wako ni mpana.
Yes, from your story, alichofanyiwa mwenye Bajaji si sawa, lakini hata wewe ulichofanya si sawa. Kwenda kuongea na dereva wa Bajaji kweli ulitegemea nini? Kwanini hukwenda kuwaona wausika moja kwa moja?
Kwa maoni yangu: Ungeenda moja kwa moja ukaomba kumuona meneja wa Mlimani city na kumuuliza kama kuna sheria/utaratibu huo ambao umewekwa na wao. Au ni walinzi waliamua kuweka utaratibu wao. Iam sure huyo meneja angekupa jibu sahihi na wewe baada ya hapo ndo ungefanya conclusion kuwa either kuna ubaguzi au vipi.
So next time ukiona tatizo kama hilo..siyo kuja JF na kumwaga "the dataz za ubaguzi wa makaburu". Do something siyo kulalamika tuu. Huwezi jua hata huyo meneja wa Mlimani City anaweza kuwa hajui walinzi kama wanawanyanyasa watu wa bajaji... Kwa kufanya hivyo, ungekuwa umewasaidia madereva na perhaps yule boss angeona kwamba kuna watu waelewa kwenye nchi yetu ambao wanafuatilia mambo. Na indirectly, ungekuwa umesaidia wengi dhidi ya manyanyaso ya walinzi..
Jamani changes ni initiave zetu wenyewe...Tusipende kulaumu tuu kwa yale ambayo we can influence changes.
Mada yako hapo juu, inaweza kuwa na ukweli, lakini ukiangalia..ni ule ule mwendelezo wa watanzania wa "kupenda kulaumu"
NEXT TIME, DO SOMETHING!
Masanja,
Kama mambo ni hivyo sishangai kwa sababu kuna wakati yaliibuka malumbano baina ya uongozi wa UDSM na wanafunzi waliokuwa wakihoji umuhimu wa mradi huu. Wanafunzi walikuwa wakidai kuwa mradi hauna uhusiano wa moja kwa moja na core function za chuo na hauna faida ya moja kwa moja katika shughuli za chuo hicho.
Inawezekana kuwa ten percent ndiyo imeshawishi watu kusaini contract ya mradi huu
Mkuu cha kusikitisha zaidi yale majengo yenyewe si imara wameweka mabord tu ya mbao kwa hiyo tutegemee baada ya hiyo miaka 50 yatakuwa yamesha oza na kuharibika na wao watakuwa wamesha pata faida mara dufu....sisi tunaachiwa gofu tu.
Ush...usijali ilikuwa usiku kwa hiyo sikuweza kupata maelezo.
Dereva wa bajaj wa kituo cha Mlimani city aliniahidi kwamba leo atafanya initiative ya kwenda kwenye vyombo vya habari na mimi nikaahidi kucreate awareness through JF.
Of course kitakachofuata utakiona...huu ni mwanzo ....Ijumaa njema
Nadhani ujenzi wa mbao haimaanishi kuwa jengo halitadumu. Tuangalie mfano wa Sweden au Marekani.
Nadhani ujenzi wa mbao haimaanishi kuwa jengo halitadumu. Tuangalie mfano wa Sweden au Marekani.
kuna wakati wezi wa power window walibuni mtindo wa kupita kwenye parking arkade kubwa kubwa kama mlimani na sea cliff kwa kutumia bajaj...wakifika wanapaki na magari wanaiba power windows ,side mirror,taa ets ..then wanatokomea..na bajaj ikitokomea dakika huipati kwa kuwa inapenya sana...
hata taxi haziruhusiwi kupaki ndani huwa zinapaki nje...
Vidada vyetu navyo vimezidi kuwinda wazungu vinatutia aibu ndio maana wanafukuzwa.......mimi siwezi kwenda sehemu kuna vidada vya aina hiyo nikiwa na mgeni wangu.....Wa akina dada hata kama anaenda kutumia pesa zake atahisiwa uchangudoa kwa sababu tu ni mwafrika.