Mlinzi wa Bobi Wine alifikishwa mahakamani Jana akiwa katika hali mbaya ya kiafya

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Mlinzi wa Mwanasiasa wa Upinzani Nchini Uganda Bobi Wine, Edward Ssebuufu maarufu kama Eddie Mutwe, alifikishwa mahakamani Jana akiwa katika hali mbaya ya kiafya akiwa anatetemeka na kulia kama mtoto…, akisaidiwa kutembea kutokana na majeraha aliyoyapata akiwa rumande. Mawakili wake walieleza kuwa aliteswa vibaya na alikuwa hawezi kusimama mwenyewe, hali iliyowatia wasiwasi kuhusu afya yake .

"Amesema mateso anayoyapitia huko rumande, anajuta kuzaliwa…Kila siku anameza vidonge 12 vya kutuliza maumivu sababu ya mateso jela… Anapigwa sana!… Makovu mwili mzima na hicho kidole sijui ndio kimekatwa " 🤷🏾‍♂️🥹

General Muhoozi Kainerugaba, Mkuu wa Majeshi na mwana wa Rais Yoweri Museveni, alidai kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye ndiye alimteka na kumtesa Mutwe, akiongeza kuwa alimkamata kama panzi na kumuweka katika hifadhi yake binafsi, jambo lililosababisha hasira kubwa miongoni mwa umma.

"Yuko kwenye chumba changu cha chini katika nyumba yangu... Na wewe unafuata!," Kainerugaba aliandika kwenye chapisho akimjibu BobiWine kuhusu kutoweka kwa Mutwe.

"Inabidi Nimhasi," alisema saa chache baadaye, na kuongeza kuwa atamwachia Mutwe pindi tu Museveni atakapotoa Amri hiyo.

Eddie Mutwe alitoweka Aprili 27 baada ya kukamatwa karibu na mji mkuu wa Kampala na watu wenye silaha, kimesema chama cha National Unity Platform (NUP) Amefunguliwa mashtaka ya uhaini na wizi wa kutumia nguvu.

Mudumoh 🤔

#halisinewsflash #h
FB_IMG_1747841268958.jpg
alisimediatz
 
#halisinewsflash #hView attachment 3341256alisimediatz
Mu7 na mwanae watakuwa na mwisho mbaya sana....Mungu hautie adabu huu utawala dhalimu na uangamize kabisa.
 
Natamani ifike siku museveni apinduliwe awekwe jela maisha yake yote yaliyobakia na mwanae akatwe kichwa kichwa hadharani kwa ushenzi wanao wafanyia waganda wenzao
 
Kweli kabisa..ila ndio ivyo mungu ni kama anawalinda maana hayawafiki madhila yoyote hao madhalimu
 
Na wakati mwingine, kuishi kunamaanisha kushuhudia hofu kabla hata ya kujua amani ni nini
 
Natamani ifike siku museveni apinduliwe awekwe jela maisha yake yote yaliyobakia na mwanae akatwe kichwa kichwa hadharani kwa ushenzi wanao wafanyia waganda wenzao
Ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom