PreGE2025 Mlinzi wa Freeman Mbowe aonekana kwenye Mkutano wa CHAUMMA unaopokea viongozi wa G55

PreGE2025 Mlinzi wa Freeman Mbowe aonekana kwenye Mkutano wa CHAUMMA unaopokea viongozi wa G55

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hivi kwani siku hizi Mbowe anahitaji ulinzi? Sasa Mbowe yupo nje ya nchi hao walinzi wanalinda nini? Nani awalipe? Hao nao wanasaka nafasi maana mshahara walikuwa wanalipwa na chama
 
Wakuu!

Mlinzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ajulikanaye kwa jina la Hassan Bwire, ameonekana akihudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) leo, Mei 19, 2025.

Sasa kama alikuwa mlinzi wake zamani anahusikaje na Mbowe sasa? Labda naye ni miongoni mwa G55.
 
Weka akiba ya maneno, mkuu. Huyu ni mwenyekiti mstaafu ujue.

Tena ni miongoni mwa waasisi wa Sidiemu nasikia.

Heshima iwepo basi, hasa tunapoelekea katika uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu.
Itifaki imezingatiwa. Sijakurupuka.

Mbowe kama mwenyekiti mstaafu na Mzee wa Chama alipaswa kutoa kauli kuhusu kushikiliwa kwa Lissu na Usaliti unaoendelea.

Sad, Hajafanya hivyo . Mara ya mwisho nilimnukuu akasema Hali ya chama ikiwa ya kutatanisha anaigia mzigoni. Kiko wapi ?

Probably Mbowe bado Yuko kwenye harakati za kuhujumu chama .
 
Wakuu!

Mlinzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ajulikanaye kwa jina la Hassan Bwire, ameonekana akihudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) leo, Mei 19, 2025.

Kama Naibu Katibu Mkuu na Mweka Hazina wamejiunga huko, unashangaa nini kumuona mlinzi? Acheni demokrasia itamalaki, hakuna haja ya kuchungulia sijui nani ameenda wakati wakiwa CDM hawatakiwi
 
Kwahiyo bwana Bwire mkono ushindwe kwenda kinywani kisa tu anatoa huduma ya ulinzi?

Be Smart!

Ndio yaleyale ya CCM ku frame kesi wale makomandoo walinzi wa Mbowe.

Hao watu kazi yao ni kutoa ulinzi, mambo yq uanachama yapo kwenu.
 
Itifaki imezingatiwa. Sijakurupuka.

Mbowe kama mwenyekiti mstaafu na Mzee wa Chama alipaswa kutoa kauli kuhusu kushikiliwa kwa Lissu na Usaliti unaoendelea.

Sad, Hajafanya hivyo . Mara ya mwisho nilimnukuu akasema Hali ya chama ikiwa ya kutatanisha anaigia mzigoni. Kiko wapi ?

Probably Mbowe bado Yuko kwenye harakati za kuhujumu chama .
Usikute anaandaa press release kama wakati ule wa Magufuli kipindi cha korona.

Naomba tujipe muda ili tupate majawabu yasiyo na chembe ya mashaka.
 
Yupo sahihi, saamsa angemlinda nani na bosi wake hayupo tena!
 
Wakuu!

Mlinzi wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ajulikanaye kwa jina la Hassan Bwire, ameonekana akihudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) leo, Mei 19, 2025.

Ruksa kwani CHADEMA ni baba yake na mama yake? Nyerere Mwenyewe alitamka wazi kuwa CCM aliyoanzisha sio baba yake na mama yake

Hata Mbowe akienda CHAUMMA ni haki yake kidemokrasia CHADEMA sio baba yake wala mama yake hajavunja katiba ya nchi
 
Probably Mbowe ni miongoni mwa Viongozi washenzi kuwahi kutokea CDM .

Probably!!
Sio yeye tu hadi mkwe wake.

Pesa ni sabuni ya roho, kanunuliwa hadi mzee wa ubwabwa, je tuendelee kuwaamini wanasiasa?
 
Mbowe kashastuka, anataka kulinda heshima yake CDM.

Hao wahuni 05 vinara wacha waende, dili la msajiki hilo.
 
Back
Top Bottom