Mlio karibu na msemaji wa Simba sc (Ahmedy Ally) muamsheni kutoka usingizini

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Baada ya pira papatu papatu na Simba sc kufuzu hatua ya makudi.

Kituo kimoja Cha redio kilifanya mahojiano na msemaji wa CAF (Ahmedy Ally) Kama anavyojiita.

Maandishi : "mashabiki wanasema kuwa wanashinda Lakini Hawana furaha!?

Ahmedy Ally: "Cha msingi kusonga mbele tutamfunga Al Ahly hivyo hivyo mpaka tutafika nusu fainali na ndiyo malengo ya Simba sc.

Maoni yangu: Ahmedy Ally anaongea kiushabiki sana na kuona mashindano ya klabu bingwa ni Kama kombe la mapinduzi, Ngao ya jamii au anadhani Kuna Coastal Union huko.

Na ndiyo maana mashabiki wanazomea timu isipopata matokeo kwa kuwa wanaaminishwa vitu ambavyo vipo nje ya uwezo kiuhalisia Simba sc kwa mwenendo huu ni ngumu kwenye makundi.

Mliokuwa karibu na Ahmedy Ally mwambieni achuje vitu vya kuongea asiongee kwa kuwapa mashabiki moyo maana football ni mchezo wa wazi.
 
Jamii Forum imevamiwa na mataaaahira MATATU.

1.........................
2.........................
3..........................
 
Timu ya madunduka kwasasa ni kama timu za UMITASHUNTA.kocha anapanga watu kwa mazoea. Msemaji analopoka inaonekana mpira haujui kabisa.
Kiufupi Ni shagalabagala.
Ila kwa mtazamo wangu kocha sio mbaya , nyota yake ndio tatizo.maana analaumiwa na kuchukiwa bila ya sababu ya msingi saana.mana kama kufanikiwa kafanikiwa kwa 70%.
Ila huyu mwanzishi wao hiyo nafasi haimtoshi kabisa.
 
Kweli Dogo anaujinga fluni hivi, anajua kuongea bila kufikirisha kichwa yaani ki mc mc hivi, hajauvaa utasasi wa simba any huenda wao ndiyo wanapenda mtu wa kariba hiyo
 
Simba haina shida yoyote shida kila alioop simba anataka kushindana na Yanga hapolazoma utamuona simba.

Ukilinganisha Yanga na Simba nikujitafitia matatizo ya pressure hivi unawezaje kumlinganisha Gamondi na Roberthno hapo lazima itendeke kwakweli.
 
Kweli kabisa [emoji16]
 
Kweli Dogo anaujinga fluni hivi, anajua kuongea bila kufikirisha kichwa yaani ki mc mc hivi, hajaufaa utasasi wa simba any huenda wao ndiyo wanapenda mtu wa katiba hiyo
Kuna watu wanampigia makofi nakumuona yupo sahihi
 
Kiburi na majivuno mwisho wake si mbali
 
Wewe ndio hujui kazi ya kuwa msemaji?
Moja ya kazi ya kuisema timu ni kuwapa moyo mashabiki na kutowakatisha tama...

Au ulishawahi kuona msemaji wa Serikali akiishishua serikali na unaona kabisa umeme ulikuwa unakatika, lakini ukienda kumuuliza atakwambia tunaendelea vizuri.

Wewe ndio unataka kumpangia cha kusema, au tukupe wewe usemaji
 
Kwa hiyo ndiyo useme utaifunga Al ahly nje na ndani wakati kiuhalisia kikosi chako Tia maji TIA maji.

Football ni mchezo wa wazi.
 
Kwa hiyo ndiyo useme utaifunga Al ahly nje na ndani wakati kiuhalisia kikosi chako Tia maji TIA maji.

Football ni mchezo wa wazi.
Anafungwa Barcelona na timu ndogo tia maji tia maji, kwa nini ishindikane kwa Al Ahly... Football ni mchezo wa wazi lakini haimaanishi uwezi kufungwa...

Kazi ya msemaji ni kutoa hamasa na si kuvunja moyo... Nitajie msemaji ya timu, taasisi, serikali au shirika lolote Duniani ambaye uwa anaponda taasisi ata ikizengua?

Usemaji sio kazi ya Udaku, ni kazi professional na wanaenda semina ya kuelekezwa nini cha kusema na nini si cha kusema...

Msemaji akianza kuponda simba ni mbovu wewe unahisi nani atanunua Ticket mchezo hujao, wengi wataanza kuichukia timu.

Hujui misingi ya usemaji, kaa kunywa uji tulia
 
Yule aliyesema mashabiki wa Simba ni mbumbumbu kweli hakukosea
 
Maoni yangu: Ahmedy Ally anaongea kiushabiki sana na kuona mashindano ya klabu bingwa ni Kama kombe la mapinduzi, Ngao ya jamii au anadhani Kuna Coastal Union huko.
Mkuu, una ujasiri gani wa kumfundisha kiongozi yeyote wa Simba kuhusu mashindano ya Klabu Bingwa? 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…