MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ilikuwa siku ya Ijumaa, tarehe 01, desemba 2001, katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi tulipokutanika wanafunzi wa kidato cha pili katika kilele cha siku ya ukimwi duniani. Shughuli zilikuwa nyingi pale lakini mojawapo ya mambo yaliyoweka alama mpaka kesho katika waliokuwepo ni kile kiapo cha hiari walichoapishwa wanafunzi kwamba hawatafanya kabisa mapenzi hadi watakapoingia kwenye ndoa.
Kwa mnaokumbuka ni kwamba siku moja kabla wanafunzi wa Old Moshi, Majengo, Pasua, Moshi Technical, St Mary Goreth, na shule zingine za Moshi zilizokuwepo miaka hiyo tuliletewa fomu ya kujaza na kueleweshwa kwamba kile ni kiapo ambacho tutaapa kesho yake pale uwanjani. Mimi niliisoma ile fomu kwa makini sana na nikaona ni jambo jema ila kutokana na imani yangu ya kutopenda viapo nikairudisha fomu siku hiyohiyo bila kuijaza. Nakumbuka wengi sana waliapa kesho yake.
Nauliza ndugu mliokuwepo na mkaapa ilichukua muda gani kuvunja kiapo?