Mliobobea katika 'Saikolojia' na 'Maono' kwa 'Msisitizo' wa 'Kauli' ya Rais Dkt. Magufuli mnamwambiaje 'Prime' Majaliwa?

Hakika uliyogundua juu ya hili jiwe la Chamwino ndo ilivyo.
 
Je, yeye ana uhakika wa kumaliza mitano tena? ICC wamekiri kupokea mzigo
Wewe uliwahi kusikia ama kuona wapi Rais wa JMT anashtakiwa wakati au baada ya Urais wake?

Tatizo vijana mnaivamia siasa bila kujipa muda wa Kupitia mawili matatu yanayohusiana na siasa. Maana hata katiba ya nchi yenu tu siku hizi hamuijui .
 
Kumbe alimtumia meseji ya kujipendekeza ya pongezi..mara ooooh umeapa vizuri lakini jiwe hakujibu ..

Kuna kitu
Mmeanza urogi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji28]
 
Ila jiwe mdomo wake hauna breki jamani..yeye na lisu wamekutana waropokaji sana.
 


My take:

Kwa kwa Cardinali Pengo kuongea maneno hayo hadharani ni haki yake na yupo sahihi kulingana wajibu wake wa utumishi wa kiroho katika jamii

Kwa Palamagambo Kabudi ni Mtaji wa kujikuza kisiasa hadharani, yawezekana aliyoyasema ni kweli lakini watu (wenye busara) watajiuliza kwanini na kwa faida ya nani waziri kama yeye aongee maneno hayo yanayohusiana na utendaji wa kazi yake na kazi za wengine???--- kumbuka sio kila jambo la UKWELI linaweza kutamkwa hadharani, na hata kama hatotamka huo ukweli hadharani je ni kwa kiasi gani tunaweza kuingia ndani ya moyo wake tujue kwamba anaishi na hayo aliyoyasema (he lives the talk)??, ndiyo maana nikasema most probably hayo maneno yake ni political milestone yaani anajifagilia njia yeye mwenyewe.

Historia ya Kabudi inaonyesha ni mtu wa kujikomba (Sycophant) kwa mkubwa, kama utakumbuka alipata kusema; Rais Magufuli kamuokota jalalani, hakika haiingii akilini kwa Profesa kama yeye kutamka maneno yale, watu tunahoji; jalalani ni wapi?, je huko jalalani alikuwa akifanya kazi peke yake???, na je huko jalalani alikuwa akifanya kazi ipi??, "takataka" za huko jalalani ni zipi???7----- sasa utaona kwa muktadha huo kauli yake ya kujidhalilisha, japo yeye anaiona ni ya kujinyenyekeza kwa mkubwa, inawatusi watu wengi sana waliopo huko "jalalani" alipookotwa na Magufuli.

Shida nyingine ya Prof Kabudi ni kuonyesha picha ya udini waziwazi katika maeneo ya shughuli za kiserikali mfano ni hiyo nukuu ya Haruni, tunajua Serikali haina dini (Neutral/ secular) kwa maana serikali ipo kwa ajili ya watu wote wenye dini na wasio na dini, sasa anapokuwa, saa zingine, ananukuu bila aibu vifungu kutoka Biblia katika shughuli za umma/kiserikali bila kujali kwamba wanachi wanaomsikiliza wanazo dini tofauti, sasa hiyo ni ishara ya udini, na mtu wa aina hiyo akipewa madaraka ya Uraisi kamwe hatoficha makucha ya udini na bila shaka ataipasua nchi vipande viwili kidini. Tz ni rahisi sana kupasuka kidini kuliko kupasuka kikabila. Kabudi ni mdini.
 
Mwenye kujua ni Mungu tu!Kwani yeye ana uhakika gani wa kuimaliza hiyo miaka 5? Anaweza akakutwa na mauti akamwacha Majaliwa akiendelea.
 

Umeandika hisia zako zaidi ya kile alichoongea Kabudi. Na sababu hizo ni hisia kwa mtu unayemuona tuu zinaweza kuwa sahihi au zisiwe sahihi.
Kuhusu hilo la udini nakataa, na nakushauri uijue familia ya kabudi kwanza, ujue familia ile yenye wakristo na waislam wanaoishi kwa upendo na amani kubwa.
 
Kiufupi tu ni kwamba Profesa Kabudi ni 'hypocrite' na 'sycophant' aliyetukuka na katika 'point' yako ya kuwa ni 'Mdini' pia nakubaliana nawe 100%.
 
Yamkini alimteua kwa shinikizo.
Tena la SSIT ili wao kwa muda huu waendelee Kumfanyia 'Vetting' vizuri Yule ambaye wanaona anafaa na ataendana vyema na 'Kasi' ya Rais JPM.
 


Mimi sijandika kwa hisia bali kwa hali halisi ya mtu mwenyewe. Hebu chukua huu mfano halisi kutoka katika kauli zake ulizoziweka hapa wewe mwenyewe:- (nakunukuu wewe) ulipoleta kauli hii ya prof Kabudi akizungumzia juu ya kutoa ushauri kwa Kiongozi mkuu (Rais) na anasema: "-------- na akiamua tofauti na ushauri wako usinune utekeleze kama vile hukuwahi kumshauri tofauti na alivyoamua----", mwisho wa kunukuu.


Kwa kauli kama hiyo unaweza kusema kweli huyo ni profesa au reverend??!!----- ilipaswa aseme hivi; "----- na akiamua tofauti na ushauri wako usinune utekeleze kama vile hukuwahi kumshauri tofauti na alivyoamua vinginevyo kama hukubalini naye kwa maslahi mapana ya taifa na ustawi wake yakupasa ujiuzulu"

Hayo maneno niliyoyaongeza katika kauli ya Kabudi uliyotuletea ndiyo haswa yanayojenga uzalendo na kujiamini kwa mtumishi kama yeye, yanajenga "integrity and magnanimity" ya mtu, hayaonyeshi KUJIKOMBA kinyume na kauli yake ya mwanzo.

Angalia hatari ya kauli yake:-

Mfano, kunapotokea mahitaji ya aina mbili katika nchi, mahitaji ya zana za kilimo na mahitaji ya dawa za binadamu, mahitaji yote hayo yanagusa ustawi wa jamii, Kabudi akae na ashauriane na mkuu wa nchi juu ya ni hitaji lipi lianze kushughulikiwa kutokana na fedha iliyokuwepo, kwa akili ya kawaida tu hitaji muhimu katika hayo mawili ni madawa, sasa kama Mkuu atasema; "hapa kazi tu, tununue vifaa vya kilimo" kinyume na ushauri wa kabudi wa kununua madawa, basi kabudi hatokuwa na njia bali kutii na kunyenyekea maamuzi ya mkuu, hatari ni hii; kwa kukosa madawa maisha ya watu yapo hatarini kiafya na maisha ya watu wengi yanaweza kupotea katika hali hiyo nani atatakiwa kuwajibika???, bila shaka wote wawili mshauri na mshauriwa, ili mshauri ajinasue kwenye mtego wa lawama ilitakiwa ajiuzulu pale tu ushauri wake ulipokataliwa na hapo atakuwa kaonyesha uzalendo na kalinda heshima yake na legecy pia.

Kuhusu udini nasema hivi; prof Kabudi mara kadhaa katika hafla za kiserikali amekuwa akinukuu vifungu vya Biblia, kwa wadhifa wake na kazi yake hapaswi kuingiza jambo lolote la kidini, kufanya hivyo ni sawa na kufanya mahubiri ya kidini kazi ambayo ni ya Wachungaji, priests (Clergies), masheikh nk.

Inatakiwa anukuu vifungu vya Biblia katika mikutano yake binafsi ya kiraia lakini sio katika dhifa na khafla za kiserikali.

Kuwa na familia yenye Wakristo na waislamu hiyo haiondoi udini wa mtu kwani dini ni imani ya mtu binafsi wala sio jambo la kifamilia.
 
All in all Waziri Mkuu wa KMajaliwa ni wa jina tu sioni kwa vitendo kama angeweza kufananishwa na waliotangulia. Kimsingi kuna Mawaziri wana influence na nguvu kwa Magufuli kuliko KMajaliwa.
 
Kama una sifa za yule tambua kwamba hufai hata kuongoza familia ile ni big mistake ilifanyika tu na waliosababisha nadhani wameshajuta kwa namna zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…