Mtazamo wangu ni huu, na nipo huru kukosolewa.
1----- Magufuli na Majaliwa wapo tofauti katika mitazamo na utendaji kazi kwa neno jingine hawaivi, jambo hili limo ndani (inside issue).
2---- Watu walishaanza toka zamani kabla ya uchaguzi kwamba Majaliwa hatorudi katika uwaziri mkuu hivyo Magufuli alishasikia hizo tetesi, tabia ya Magufuli ni siku zote kwenda kinyume na tetesi za watu, yaani hapendi kufuata kile kinachosemwa na watu na ndiyo maana Kamrudusha tena Majaliwa kwani asingemrudisha ingeonekana kasikiliza na kafuata tetesi za watu.
3---- Magufuli anamtafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi ya Majaliwa ndiyo maana kisha mpa taarifa mapema ajiandae kisaikolojia na pia hiyo ni huruma au hisani au shukurani aliyopewa ya muda mfupi atakaokaa katika cheo cha uwaziri mkuu kwani ni mambo "makubwa" wameyafanya pamoja katika uchaguzi mkuu uliopita, mambo ya kupora haki za wananchi kujichagulia wapendacho, bila shaka siri za mambo yaliyofanyika wote wanazijua.
Kwa kauli hizo za Magufuli juu ya Majaliwa ni sawa na baba kumwambia mwanaye; Jirekebishe ama sivyo nitakuadhibu. Nimechoka na tabia na utendaji wako nikimpata mtoto mwingine atakuja shika mahala pako.
Pia dini ni kinga kwa Majaliwa katika nafasi hiyo ya waziri mkuu, kwani tayari tetesi zimekuwepo kwamba watu wa dini fulani wanapendelewa katika nafasi za uwaziri.
****Nahofia watu watakuja na povu mdomoni.🤣✊🏻✌🏻✌🏻✌🏻✌🏻