Mlioenda kijijini kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu nyoosheni mikono juu!

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Watu wengi hupendelea kurudi makwao, hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Wengi hurudi vijijini ambapo ndipo chimbuko lao lilipoanzia, ili kusherehekea kwa pamoja; wapo wanaochinja mbuzi, ng'ombe n.k ili mradi kunogesha furaha ya kuwa pamoja na kujiandaa kukaribisha mwaka mwingine.

Lakini cha ajabu, kuna wengine wapo mjini tu, miaka nenda miaka rudi; wanasema wako bize kutafuta hela.

Sasa nataka niwaulize; nyie hamna makwenu, chimbuko lenu liko wapi? Au ni sababu zipi zinazokufanya usiende kujumuika na chimbuko lako?
 
Screenshot_20221219-125402.png
wazee wa kuroga na matambiko sisi hayo mambo hatuna mshaanza kumaliza na magorofa huko.

Angalia hao vijana utajua huko ni walevi kwa sana. Jua kali Makoti makubwa
 
Watu wengi hupendelea kurudi makwao, hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Wengi hurudi vijijini ambapo ndipo chimbuko lao lilipoanzia, ili kusherehekea kwa pamoja; wapo wanaochinja mbuzi, ng'ombe n.k ili mradi kunogesha furaha ya kuwa pamoja na kujiandaa kukaribisha mwaka mwingine.

Lakini cha ajabu, kuna wengine wapo mjini tu, miaka nenda miaka rudi; wanasema wako bize kutafuta hela.

Sasa nataka niwaulize; nyie hamna makwenu, chimbuko lenu liko wapi? Au ni sababu zipi zinazokufanya usiende kujumuika na chimbuko lako?
Sie kwetu mjini tu. Hatuna pa kwenda tunabaki kuendelea kutafuta karo za shule na muendelezo wa sikukuu zijazo.
 
Back
Top Bottom