Mliofanikiwa kuacha kazi na kujiajiri mlitumia mbinu gani?

Labda uvivu tu wa kutowafatilia vijana.
Ukiacha kazi ukaisimamia mwenyewe biashara bado utawahitaji vijana tu wa kukusaidia eidha usipokuwepo au wa kukusaidia ukilemewa.

Cha kufanya mi nakushauri usiache kazi, bado unaweza kupiga hatua ukiwa hukohuko kazini. Ni vile unalea vijana wanaokupa hasara. Labda una huruma sana mkuu, hesabu ni njia nzuri ya kumkamata mwizi kwenye biashara.

Inawezekana wewe ni moja ya wafanyabiashara "wakabia macho" yaani yeye akifika dukani anaangalia shelf kama lina vitu basi roho kwatu anajua biashara iko safi.
Hufanyi stock, unaenda kuwapokea vijana ukitoka job bila makabidhiano ya hesabu yoyote zaidi ya fedha tu.
Hapo hata kama vijana sio wezi ila unawatamanisha waibe, na wataiba kweli.
 
Labda uandike barua kwa mkurugenzi ukiomba rikizo ya mwaka bila ya kulipwa mshahara,ruhusa hii ipo kwa wafanyakazi wa serikalini hasahasa walimu
Nakazia ✍️✍️
Baada ya mwaka atapata jibu sahihi kutokana na performance ya biashara yake
 
Uko sahihi kama haupo kwenye field ya biashara ya duka unaweza kumsena mmiliki,hii ni biashara inayohitaji usimamizi wa juu sana,mfano mauzo yangu yanarange 2-3ml per day Kuna mfanya alikuwa alikuwa anachukua 15000 Kwa siku nikikuja nikamkuta amesave mil 1.5,hata maduka madogo bila mmiliki kusimamia ni hatari,off course nafukuza sana lkn haileti stability ktk biashara
Sasa mtu kakuibia 1.5 m unajua nyuma aliiba ngapi[emoji848] kamata weka ndani huyo mtu akili imkae sawa....., Halafu kwa biashara kama hyo tayari ni kubwa mbn kuna app nyingi za kucontrol biashara
 
Sio wote wamefanikiwa kuwa na biashara
Lazima ujue ya kuwa kama umefikia hatua ya kuwa na biashara tena aina tofauti, basi umefika pazuri sana na utaendelea zaidi

Kuhusu kazi yako hiyo huna ulazima nayo ila ni uoga wako tu
Usichanganye biashara na kazi unless una partners wenye shares sawa na wewe

Lakini kama ni zako basi acha kazi enedelea kuza biashara zako na ukizisimamia vizuri utaendelea sana kwa moyo mmoja na mtangulize Mungu sana na umuombe sana na kama humuamini basi hata mizimu yenu sawa tu

Hakuna aliefika mahali bali bahati tu na jitihada zake
Ukiacha kazi unaweza kuongeza biashara ambazo utazimudu kuzisimamia kila siku

Nakuombea mafanikio mema
Na kama una ndugu ambao unajua wanakuhitaji kila mwezi na wanaweza kujituma basi wape kazi upate Baraka zao
 
Biashara zina nyakati, sio kila siku zitafanana.

Kuna mtu alikuwa na biashara ya vyakula kubwa sana hadi kuna wakati alivamiwa kutokana na hesabu kubwa aliyokuwa anafunga kwa siku.

Ilitokea ya kutokea lile eneo likavunjwa kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa barabara.

Alihamisha biashara yake sehemu tofauti kidogo na pale na hakuweza tena kupata hesabu hata nusu ya aliyokuwa anapata.

Huo ni mfaano tu ni sawa na ununue bajaj alafu iibiwe ikavunjwe vunjwe huko.

Tafuta vijana waaminifu pia funga camera zitasaidia kuweka umakini lkn pia waambie ukweli na uwaambie wakishindwa kuwa waaminifu hutaweza kuendelea nao.
 
Asante mkuu,Kuna muda najiona bwege sana honestly,kiuhalisia Pato langu la biashara ni mara Tano ya mshahara lkn hofu IPO juu balaa
 
Huo uoga wenu utawafikisha pabaya, unalipya sh 600k kwa mwezi ambao ni wasitani wa sh 20k kwa siku, na huna uhuru, utaacha je kazi yako kwa vijana inao kuingizia 50k kwa siku ambao ni 1.5m.........kama sio economic ignorance ni nini hiyo? Kisa eti nina bima ya afya foolish kwani unaugua kila siku?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ni wanaume wachache wenye uamuzi wakijasiri wa kuacha kazi ya serikali yenye unyonyaji, kama hauko miongoni mwahao uta shinda mitandaoni kuomba ushauri, hasa ukiwa unatoka familia masikini za wakulima kufikia maamuzi sio rahisi, mimi niliacha hiyo kazi ya kishezi mwaka 2007 sijawahi kujutia na sioni mtumishi tuliokua nae anae nizidi, labda majungu na fitna ndo wanazo nizidi........huwezi kupata maisha mazuri ukiwa mualimu wa darasani hapa Tanzania its a big joke.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Biashara zina nyakati, sio kila siku zitafanana.

Kuna mtu alikuwa na biashara ya vyakula kubwa sana hadi kuna wakati alivamiwa kutokana na hesabu kubwa aliyokuwa anafunga kwa siku.

Ilitokea ya kutokea lile eneo likavunjwa kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa barabara.

Alihamisha biashara yake sehemu tofauti kidogo na pale na hakuweza tena kupata hesabu hata nusu ya aliyokuwa anapata.

Huo ni mfaano tu ni sawa na ununue bajaj alafu iibiwe ikavunjwe vunjwe huko.

Tafuta vijana waaminifu pia funga camera zitasaidia kuweka umakini lkn pia waambie ukweli na uwaambie wakishindwa kuwa waaminifu hutaweza kuendelea nao.
100%,Biashara huwa ina sifa moja kubwa ya kuwa kigeugeu,watu wengi wasio na experience ya biashara hawawezi kujua hili.
 
Niliajiriwa 2014 kwenye sector ya elimu(mwalimu),nimepambana na maisha ya utafutaji Si haba Mungu kanisaidia nimefanikiwa kupata mtaji kiasi,nimefungua maduka mawili,duka la mahitaji ya nyumbani jumla na rejereja na la pili ni duka la simu,vifaa vya umeme na huduma za fedha mtandaoni((mpesa,tigo pesa n.k).
Duka Moja anasimamia make wangu na la pili nimeajiri vijana watatu,NAMI nikitoka kazini huwa naingia kazini kusaidia duka mojawapo,katika kufanya kazi huko nakumbana na changamoto nyingi.
Kukosa uaminifu kwa vijana,usimamizi hafifu wa kazi,kupitia changamoto hizi naona ukuaji wa biashara ya Si kama vile ninavyotegemea na hili naliona hasa kipindi Cha likizo nikiwepo mwenyewe biashara yangu huwa inaimarika sana.
KWENU WAUNGWANA;Kuna muda nawaza kusitisha ajira yangu nijikite katika biashara kwani kupitia huko ntajikwamua kiuchumi zaidi,Si Kwa kudharau ualimu la hasha kwani kupitia ualimu ndo nimepata mtaji Bali ualimu huu naona hautanisaidia kufanikiwa zaidi,huwezi kuajiri mtu akutafutie million 100 ww ukabaki unatafuta laki 6 ya ualimu.
Kila ninapofikiria kuacha kazi napata mkwamo mkubwa wa mawazo,lkn pia napata msongo mkubwa wa mawazo Kwa kutotimiza majukumu yangu ya ualimu vizuri,mara nyingi natoroka kazini Kwa kifupi sitekelezi majukumu yangu ipasavyo na ni dhambi kubwa naifanya,Kwa wanaoujua ualimu vizuri Ili utekeleze majukumu Yako yote hautaweza kujihusisha na shughuli zingine.
Mliofanikiwa kuacha kazi na kujiajiri mlitumia mbinu gani,msaada tafadhari Ili nijikwamue kutoka katika hili
Unawaza nini omba likizo isiyo na malipo ya mwaka mmoja (zingizia chochote huko kazini) komaa hapo then baada ya mwaka utakuwa umepata jibu mujarabuu kabisa uendelee na kazi au ufanye biashara..
 
Niliajiriwa 2014 kwenye sector ya elimu(mwalimu),nimepambana na maisha ya utafutaji Si haba Mungu kanisaidia nimefanikiwa kupata mtaji kiasi,nimefungua maduka mawili,duka la mahitaji ya nyumbani jumla na rejereja na la pili ni duka la simu,vifaa vya umeme na huduma za fedha mtandaoni((mpesa,tigo pesa n.k).
Duka Moja anasimamia make wangu na la pili nimeajiri vijana watatu,NAMI nikitoka kazini huwa naingia kazini kusaidia duka mojawapo,katika kufanya kazi huko nakumbana na changamoto nyingi.
Kukosa uaminifu kwa vijana,usimamizi hafifu wa kazi,kupitia changamoto hizi naona ukuaji wa biashara ya Si kama vile ninavyotegemea na hili naliona hasa kipindi Cha likizo nikiwepo mwenyewe biashara yangu huwa inaimarika sana.
KWENU WAUNGWANA;Kuna muda nawaza kusitisha ajira yangu nijikite katika biashara kwani kupitia huko ntajikwamua kiuchumi zaidi,Si Kwa kudharau ualimu la hasha kwani kupitia ualimu ndo nimepata mtaji Bali ualimu huu naona hautanisaidia kufanikiwa zaidi,huwezi kuajiri mtu akutafutie million 100 ww ukabaki unatafuta laki 6 ya ualimu.
Kila ninapofikiria kuacha kazi napata mkwamo mkubwa wa mawazo,lkn pia napata msongo mkubwa wa mawazo Kwa kutotimiza majukumu yangu ya ualimu vizuri,mara nyingi natoroka kazini Kwa kifupi sitekelezi majukumu yangu ipasavyo na ni dhambi kubwa naifanya,Kwa wanaoujua ualimu vizuri Ili utekeleze majukumu Yako yote hautaweza kujihusisha na shughuli zingine.
Mliofanikiwa kuacha kazi na kujiajiri mlitumia mbinu gani,msaada tafadhari Ili nijikwamue kutoka katika hili
Tafuta namna nzr ila usiache kazi!! Ni Bora upunguze idadi ya wasimamizi hasa vijana wa3 ukabaki na mmoja unayemuona ana akili na uaminifu ndo muwe mnasaidiana.
 
Back
Top Bottom